• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU AZINDUA JENGO LA MAMA NA MTOTO AMANA, AMPONGEZA RC MAKONDA KWA KUFANIKISHA UJENZI WA JENGO HILO

Posted on: February 14th, 2018

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo amezindua jengo la Mama na Mtoto Hospitali ya Amana lililojengwa kwa jitiada binafsi za RC Makonda kutafuta wafadhili wa kampuni ya Amsons Group iliyoridhia kujenga jengo hilo pasipo kutumia fedha ya Serikali.

Ujenzi wa jengo hilo lenye thamani ya Billion 1.2 ni matokeo ya RC Makonda kuona mateso na uchungu waliokuwa wakipata kinamama waliokuwa wakijifungua kwenye jengo Dogo na Chakavu "kibanda" lililojengwa Miaka 60 iliyopita hali iliyokuwa ikisababisha kulala kitanda kimoja watu watatu hadi wanne "mzungu wa nne" na wakati mwingine wagonjwa kuja na godoro au kanga nyumbani ili aweze kuweka chini alale.

Kwa sasa kinamama wanafurahia maisha kwa kutumia jengo la kisasa la gorofa mbili na ground floor ambapo ndani yake kuna wodi za kisasa, vyumba vya upasuaji, Mahabara, vitanda vya kisasa 150 vyenye neti na makabati yake, feni,mapokezi,sehemu ya mapumziko na madirisha ya Vioo yanayoruhusu mwanga na hewa ya kutosha.

RC Makonda amesema awali kinamama wanaojifungua walilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda kutokana na kukosekana kwa jengo la kutosheleza mahitaji hivyo jengo litamaliza changamoto hiyo.

Aidha RC Makonda amesema uwepo wa jengo hilo utasaidia kupunguza idadi ya vifo vya Mama na Mtoto waliokuwa wakipoteza maisha kwa kujifungua kwenye mazingira yasiyo rafiki.

Aidha ameshukuru kampuni za Amsons Group kwa kufanikisha ujenzi wa jengo hilo na kueleza kuwa kwa sasa wanajenga jengo Kama hilo Hospitali ya Mwananyamala kisha Temeke ambapo pia kuwapongeza watumishi wote wa sekta ya afya kwa kutoa huduma bora na kupunguza malalamiko ya wananchi.

Nao viongozi walioshiriki uzinduzi huo akiwemo Naibu waziri wa Afya, Wakuu wa wilaya, Wabunge, Wakuu wa Idara, Madiwani,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na wananchi wamemsifu RC Makonda kwa kuleta ukombozi kwenye Mkoa wa Dar es salaam.

Baadhi ya kinamama wameeleza kuwa jengo hilo ni zuri na la kisasa kwa kuwa lina vitu vyote muhimu ambapo baadhi yao wamesema hawatamani hata kuruhusiwa kurudi nyumbani ambapo wamemshukuru RC Makonda kwa kuona kilio chao cha muda mrefu na kukipatia ufumbuzi.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAS MADENGE ASISITIZA UTOAJI HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI

    January 24, 2023
  • RC Makalla Kuwapeleka Safari ya Mafunzo Viongozi wa Bodaboda na Machinga Nchini Rwanda

    January 20, 2023
  • RC Makalla Atembelea Ujenzi wa Kituo cha Biashara Afrika Mashariki

    January 19, 2023
  • RC Makalla Achoshwa na Danadana za Mkandarasi Soko la Tandale

    January 19, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa