• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

WADAU WAENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RC MAKONDA

Posted on: August 2nd, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shilingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.


Makonda amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi 20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.

Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.

Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi  viongozi wote akiwemo Mheshimiwa Makonda atapata kujua.

Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.

“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.

Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa