• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Wadau Kupanda miti zaidi ya 2000 Kuunga mkono Kampeni ya RC Makalla "SAFISHA PENDEZESHA DSM"

Posted on: January 29th, 2022

- Leo Januari,29,2022 RC Makalla ameungana na wakazi wa Manzese kufanya usafi na Wadau Kampuni ya Mondi Ltd wamepanda miti 500 kandokando ya mto Mpigi Bunju B, kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa

- Waahidi kuendelea kupanda miti Zaidi ya 2000 kuunga Mkono Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM

Ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM tangu kuzinduliwa rasmi na RC Makalla leo ameungana na wakazi wa Manzese Manispaa ya Ubungo kufanya usafi, huku akiwapongeza kwa kujumuika naye katika zoezi hilo.

RC Makalla ametoa wito kwa Wakazi wa DSM kuendelea kufanya usafi ili Jiji liwe safi kwa kuwa DSM ndio lango la Tanzania, Vilevile amesema wafanyabiashara wadogo wasirudi tena Barabarani kwa kuwa kufanya biashara holela ni chanzo kikubwa cha Uchafu.

Katika kuunga mkono juhudi hizo za RC Makalla Kampuni ya Mondi LTD ambao wanajishughulisha na Usafi wa mito, kutoa taka ngumu na tope na mchanga ambao unatumika kwa Ujenzi leo wameunguna na Mkuu wa Mkoa wa DSM kufanya usafi na kupanda miti katika mto Mpigi Bunju B.

Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Francis Mondi amesema pamoja na shughuli za kila siku za Kampuni hiyo leo Januari 29, wameunguna na RC Makalla kufanya usafi na kupanda miti, leo wamepanda 500 wataendelea kupanda, huku akiahidi kuendelea kuunga mkono Kampeni mbalimbali katika Mkoa wa DSM

Aidha Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu Mkoa Dkt Elizabeth Mshote amewashukuru wadau kwa kushiriki kupanda miti na kuienzi kwa vitendo Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM pia kubuni wazo la kuwa na kitalu katika eneo la Bunju B ambacho kitasaidia kuzalisha miche ya miti ambayo itapandwa katika maeneo mengine ya Mkoa wa DSM

Ifahamike kuwa leo Januari 29,2022 ni mwisho wa mwezi ambapo kufuatia agizo la RC Makalla Wakazi wa Dar es Salaam wameshiriki kufanya usafi wa pamoja katika maeneo yao pamoja na kupanda miti Zoezi hili ni endelevu likisimamia nguzo kuu nne; kuwapanga wafanya biashara vizuri; Kufanya usafi; Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara; Kuhakikisha wafanyabiashara hawarudi katika maeneo waliyoondolewa


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa