• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

TUNAENDELEA KUBORESHA UTUMISHI SEKTA ZOTE

Posted on: July 14th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepokea Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka katika kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri unaofanywa na Ofisi hiyo.

Upatikanaji wa Computer hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya shauku na utafutaji wa Mheshimiwa Makonda kwa ajili ya kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam, ambapo itakumbukwa hivi karibuni Mheshimiwa Makonda alifanya mkutano na Watumishi wa sekta ya Ardhi wa Manispaa zote na moja ya kero kubwa iliyo bainishwa kuwasumbua wananchi ni namna ya kupata kibali cha ujenzi jambo lililomkera Mheshimiwa Makonda.

Kucheleweshwa kwa huduma ya namna hii kwa wananchi huchochea utoaji Rushwa na ujenzi holela  bila vibali unaosababisha  Serikali kupoteza kodi ya viwanja na kodi zingine zinazohusiana na ardhi.

Aidha amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipata kero mbalimbali ikiwemo ile ya kupewa kibali na manispaa kisha wakaja watu wa zima moto wakakuzuia kuendelea kwa ujenzi sababu hawana taarifa, huku wakati mwingine ukimalizana na watu Zimamoto wanakuja watu wa OSHA nao wanakuzuia usiendelee na ujenzi.

Hivyo basi badala ya hivi vitengo husika nane kuwa sehemu moja (one stop center) badala yake vimetawanyika na kuwa kero na usumbufu kwa wananchi hasa wanaotaka kufuata taratibu.

kutokana na sababu zote hizo Mheshimiwa Makonda ameamua kutengeneza mfumo mpya utakaomwezesha mwananchi kutokwenda kupanga foleni Manispaa yoyote ile anapotaka kibali cha ujenzi badala yake anaweza kutuma kwa njia ya mtandao na vitengo vyote vinane vikapokea taarifa hizo kwa wakati mmoja na kumfanya kila mwenye kitengo chake kuwajibika kwa wakati pasipokuwa na kisingizio cha kupoteza taarifa za wateja, urasimu na hata lugha mbaya kwa wananchi wanaotaka huduma ya Serikali.

Aidha mfumo huo utamwezesha Mkuu wa Mkoa kuona nani anakwamisha utendaji ili hatua za haraka zichukuliwe na mwananchi apate huduma ya haraka.

Mfumo huu pia utamwezesha mwananchi kutuma kero inayohusu huduma ya ardhi popote alipo na ikapatiwa ufumbuzi pasipo yeye kuhangaika.

Mkuu wa Mkoa ameahidi pia kuwapatia Pikipiki 50 watendaji wa idara ya ardhi  ili waweze kufanya safari za  haraka kwenda kwenye migogoro ya ardhi pale  inapoibuka kabla ya madhara makubwa kutokea.

“Nataka ifike mahali Mwananchi yoyote Yule bila kujali kipato chake akiomba kibali cha ujenzi apatiwe ndani ya mwezi mmoja, haiwezekani mtu anatuma maombi ya kupata kibali cha ujenzi anazungushwa na hatimae anakata tamaa na mwisho wa siku anajenga bila kibali na kusababisha ujenzi holela.” aliongea Makonda.

Kwa hiyo ndio maana nikaona twende kwenye mfumo wa kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi na Serikali kupata mapato. Nikimaanisha ndani ya mwezi mmoja unatosha kupitia taarifa na kupitia maombi yao ili kamati ya mipango miji ifanye kazi yake ndani ya wakati.” alisisitiza Makonda.

Sanjari na hayo Mkuu wa  Mkoa ameushukuru uongozi wa kampuni ya TAMOBA kwa kutimiza ndoto aliyonayo na kueleza kuwa sasa ni wakati wa wataalamu kukamilisha mfumo ili wananchi waanze kupata huduma ya kisasa na aina yake.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa amesema kuwa wameamua kutoa zawadi hizo kwa mkuu wa mkoa ili kusaidia kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam huku akionyesha kushangazwa na watanzania wanaoingiza chuki na ubinafsi katika kazi nzuri anayoifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Joseph Kimisha amesema kuwa kampuni yao inafarijika na namna ofisi ya mkuu wa mkoa inavyoshughulikia kero za wananchi kwa ufanisi na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na ofisi hiyo bega kwa bega.                       

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa