• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Sikukuu ya Wafanyakazi Yafana Jijini Dar es Salaam

Posted on: May 1st, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva amewaongoza wafanya kazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Mhe. Paul Makonda kwa  kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyoadhimishwa katika Uwanja wa Uhuru jijini hapo.

Awali Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Temeke alipokea maandamano ya wafanyakazi hao yaliyoanzia katika Jengo la TUCTA Mnazi Mmoja na kupita mbele yake yakiwa na jumbe mbalimbali.

Akizungumza katika maadhimisho hayo DC Lyaniva amewataka Waajiri wote katika Mkoa huo kufuata Sheria ya Ajira ya kuwapatia wafanyakazi mkataba na kudumisha Usalama wa Kazi.

Amesema wapo baadhi ya Waajiri ambao hawatoi Mkataba wa kazi na badala yake wanashikilia vyeti vya wafanyakazi hao jambo linalopelekea Waajiriwa kufanya kazi katika mazingira magumu.

"Niagize kila Mwajiri ahakikishe uwepo wa mkataba wa ajira na Usalama kazini ili kuboresha mazingira ya wafanyakazi wao kwani wasipokuwa na mkataba haki zao hawatazipa kama inavyotakiwa”.


Aidha amewataka Maafisa kazi kuhakikisha wanasimamia haki na stahili za wafanyakazi ili kutengeneza mazingira mazuri ya kazi.

Pia amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na kwa haki na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea katika  kuwahudumia wananchi bila kudai rushwa kwani rushwa ni adui wa haki na maendeleo kwa ujumla.

Hata hivyo ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma bora na kuwathamini wafanyakazi na kuhakikisha Sekta za Umma na Binafsi zinatatua kero mbalimbali za wafanyakazi.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mmbando, Wakurugenzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam, Makatibu Tawala wa Wilaya , Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini pamoja na Vyama mbalimbali vya wafanyakazi.

Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Uunganishaji wa Mifuko ya Jamii Ulenge Kuboresha Mafao ya Mfanyakazi”.

 

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa