• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makonda Azindua Kampeni ya Kuzuia Vifo Vitokanavyo na Uzazi, Akabidhi Billioni 3 za Ujenzi wa Hospital za Wilaya

Posted on: March 13th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya tukio la kihistoria la uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na kukabidhi hundi ya Shilingi Bilioni 3 alizotoa Rais Dkt.John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa Hospital za Wilaya ya Kigamboni na Ilala eneo la Kivule ambapo ametoa muda wa Miezi 3 kuhakikisha ujenzi umekamilika.

Akizungumza katika Uzinduzi huo RC Makonda amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha inapunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa vifo vya Mama na Mtoto kwa kujenga Hospital za kutosha, Zahanati, Vituo vya Afya, Ununuzi wa Magari ya kubebea Wagonjwa pamoja na vifaa tiba ili wananchi wasipate tabu.

RC Makonda amesema katika Fedha hizo Wilaya ya Kigamboni imepokea Shilingi Bilion 1.5 na Ilala Bilioni 1.5 ambapo Hospital zitakazojengwa zitakuwa na watumishi zaidi ya 500 na kuongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Hospital hizo za Wilaya pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital nyingine ya kisasa eneo la Mabwepande.

Aidha RC Makonda amewataka wanaume kuwasindikiza wake zao Clinic ili kujua maendeleo ya Afya zao jambo litakalosaidia kuepusha vifo vya mama au mtoto wakati wa kujifungua.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka mabinti kuhakikisha wanaepuka Mimba za utotoni ambazo zimekuwa chanzo cha ongezeko la vifo na hata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

 Uzinduzi wa Kampeni ya kuzuia Vifo vitokanavyo na Uzazi JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA inaenda na kaulimbiu isemayo kila mmoja anao wajibu wa kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi "MANENO BASI SASA NI VITENDO

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa