• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA AZIDI KUBORESHA JESHI LA POLISI

Posted on: September 8th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amekabidhi Pikipiki za Traffic 10, Computer 100 na Baiskel za kisasa 200 kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi la Dar es Salaam na kulifanya kuwa la kisasa.

Kupatikana kwa vitendea kazi hivyo ni matokeo ya jitihada binafsi za Mheshimiwa Paul Makonda katika kutafuta Wahisani.

Mhe. Paul Makonda amesema amedhamiria kuleta Mapinduzi Makubwa kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na Vifaa vya kutosha ikiwemo Magari, Pikipiki za kawaida na zile za Traffic, Baiskeli za Doria, Silaha na Computer ili kufanya kazi katika Mazingira mazuri.

Amesema amechoka kuona Askari wakipoteza Maisha wakitekeleza majukumu yao kwa kuvamiwa na majambazi na kuporwa Silaha ndio maana anapambana kutafuta vitendea kazi ili Askari wake wajivunie kufanya kazi katika Mkoa wake.

Aidha amesema Pikipiki za Traffic zitaenda kusaidia kwenye Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha wagonjwa Hospitali.

Kuhusu Computer 100 alizotoa amesema zitagawanywa kwenye Vituo vya Polisi 20 na kufungwa mfumo wa kisasa wa kupokea taarifa za uhalifu, kubainisha maeneo yaliyoshamiri uhalifu, kutambua wahalifu Sugu ambapo mfumo huo utatoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa, Wilaya na Mkuu wa kituo ili kuwezesha Viongozi kufanya maamuzi.

Amesema Baiskeli 200 alizozitoa zitaendelea kuimarisha Doria mitaani na kuongeza kuwa Baiskeli nyingine za kisasa 1,000 zipo nchini China zikifanyiwa Maboresho ambapo zikikamilika zitakuja kuongeza nguvu kupambana na Uhalifu.

Sanjari na hayo amesema Magari Mabovu 15 ya Polisi kati ya 26 yaliyopelekwa Kilimanjaro kufanyiwa marekebisho yamekamilika ambapo yatakuwa na mwonekano wa kisasa kama ilivyo kwa Magari ya Jeshi ya UN.

Pamoja na kuligusa Jeshi la Polisi kama Taasisi ameona pia aguse maisha ya Askari mmoja mmoja kwa kuwatafutia Mkopo wa Viwanja sababu gharama ya Viwanja ni kubwa hivyo kufanya Askari kushindwa kumudu gharama hali inayosababisha baadhi yao kustaafu wakiwa hawana makazi na kuishi kwa tabu.

 Viwanja hivyo vilikuwa vikiunzwa kwa Tsh 20,000/= kwa Square meter lakini Mhe. Paul  Makonda amepambana hadi kufikia Tsh 5,000/= kwa Square Meter ambapo Askari watakuwa wakilipa mkopo huo kidogo kidogo kwa muda wa Miaka Mitano na wataruhusiwa kujenga hata kama hawajamaliza mkopo wao

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Operesheni Panya Road Imekuwa na Mafanikio

    May 27, 2022
  • RC Makalla Asimamisha Shughuli za Uchimbaji Madini Boko - DSM

    May 26, 2022
  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa