• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA ATEMBELEA SHULE ZILIZOONGOZA KWA UANDIKISHAJI MKUBWA WA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA TANZANIA NZIMA, AAGIZA UJENZI WA SHULE MPYA

Posted on: February 21st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya Ziara kwenye Shule ya Msingi Mbande na Maji Matitu zilizopo Manispaa ya Temeke ambazo zimeongoza kwa kuandikisha idadi kubwa ya Wanafunzi wa Darasa la Kwanza kuliko shule yoyote Tanzania na kusababisha mlundikano mkubwa wa Wanafunzi Darasani.

Kwa Shule ya Msingi Mbande imeandikisha zaidi ya Wanafunzi 1,130 na kusababisha upungufu wa Vyumba vya Madarasa 115 na Matundu ya Vyoo 270 na Madawati 308 huku shule ya Msingi Maji Matitu nayo ikiandikisha zaidi ya Wanafunzi 976 hali iliyosababisha baadhi ya Wanafunzi kukaa kwenye Sakafu, Chini ya miti na Msongamano mkubwa Madarasani.

Hali hiyo imemfanya RC Makonda kufika kwenye shule hizo ili kujua mpango wa Manispaa katika kutatua changamoto hiyo iliyosababishwa na nia njema ya wazazi kuitikia wito wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ya kutoa elimu Bure.

Kama ilivyo kawaida ya RC Makonda kutafuta majibu kwenye Changamoto amesema serikali inaanza mara moja ujenzi wa shule tatu Mpya ambapo Shule mbili zitajengwa Maji Matitu na Moja Mbande.

Aidha RC Makonda amesema makadirio ya uandikishwaji wa wanafunzi wapya darasa la kwanza kwa Wilaya ya Temeke ilikuwa wanafunzi 7,800 lakini idadi imepanda hadi kufikia Wanafunzi 28,824 na idadi inazidi kuongezeka kila kukicha huku Mkoa ukiwa na malengo ya kuandikisha wanafunzi 78,000 lakini hadi sasa wamefanikiwa kuandikisha Wanafunzi 86,000.

RC Makonda amesema mwitikio huo wa wananchi kwenye elimu ni faida kubwa kwakuwa ndio ukombozi wa familia maskini hivyo amewasihi wananchi kuchangamkia fursa ya iliyotolewa na Rais Magufuli ya Elimu Bure.

Hata hivyo RC Makonda amewahimiza Wananchi kuunga mkono ujenzi wa shule hizo tatu mpya kwa kujitolea vifaa mbalimbali kama Saruji, Mchanga,  Nondo, Kokoto, Mabati, Rangi, Mbao na nguvu kazi ya Watu ili wanafunzi wasome katika mazingira bora.

Kwa upande wake kaimu afisa elimu ya msingi manispaa ya Temeke Bi. Sylvia Mtasingwa amesema licha ya shule ya Mbande kuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi imeendelea kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.

UKITAKA KUMKOMBOA MTOTO WA FAMILIA MASKINI MPATIE ELIMU, KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU DAR ES SALAAM.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa