• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makonda atangaza fursa ya Ajira kwa Vijana Waliomaliza Mafunzo ya JKT na Mgambo

Posted on: July 1st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Vijana waliomaliza mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi kufika ofisini kwake Ijumaa ya July 06 kwa ajili ya kupatiwa ajira ya kusimamia usafi na kuwatoza faini vinara wa uchafuzi wa mazingira.

RC Makonda amesema katika fedha itakayotozwa kwa wachafuzi wa mazingia 50% itaenda kwenye Halmashauri na 50% kwa vijana wa JKT na Mgambo ambapo kabla Vijana hao hawajakabidhiwa jukumu hilo watapewa mafunzo ya Sheria ya Usafi.

Huu ni Ubunifu Mkubwa aliofanya RC Makonda katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana sambamba na kuufanya mji kuwa katika hali ya usafi baada ya mbinu nyingi zilizokuwa zikitumiwa  kuhamasisha usafi kutokuwa na matokeo mazuri.

Aidha RC Makonda ameagiza makampuni yote yaliyopewa tenda ya usafi Dar es salaam kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata na Halmashauri kufika ofisini kwake Jumatano ya July 04 wakiwa na mikataba yao kwa ajili ya kujiridhisha uwezo wao wa kufanya kazi baada ya uchunguzi aliofanya kubaini uwepo wa kampuni zilizopewa tenda Kubwa wakati hawana vifaa vya kutosha.

Hata hivyo RC Makonda ameziagiza Manispaa zote za Jiji hilo kuhakikisha kila mfanyabiashara na vituo vya daladala vinakuwa na Sehemu ya kuweka taka (dustbin).

Pamoja na hayo RC Makonda ametangaza fursa kwa wadau wenye vyoo vya kuhama (mobile toilet) kufika ofisini kwake ili wakutanishwe na Halmashauri ili waweke makubaliano ya ushirikiano ili kuondoa tabia ya watu kujisaidia kwenye kuta na vichochoro.

 Miongoni mwa majukumu ya Vijana hao ni kuhakiki makampuni kwenye mitaa kama yapo na yanafanya kazi kweli, kujua wananchi wanapeleka wapi takataka, kukamata watupaji wa taka na kuwatoza faini ambapo Kama huna pesa utapewa adhabu ya kufanya usafi wiki nzima chini ya usimamizi

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • "Dar es Salaam Mmefanya Vizuri Oparesheni ya Anwani za Makazi na Postikodi" Waziri Nape

    May 18, 2022
  • RC Makalla Apokea Kero zaJumuiya ya Wafanyabiashara Dar es Salaam.

    May 16, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa