• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA APOKEA MAGODORO 1,000 APIGA MARUFUKU WAGONJWA KULALA CHINI

Posted on: September 14th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Magodoro 1,000 yenye thamani ya Shillingi Million 100 kutoka Kiwanda cha utengenezaji wa Magodoro ya Dodoma Asili kwa kushirikiana na Wadau wanaopendezwa na kazi kubwa anayoifanya katika kutatua kero  za wananchi.

Mhe. Paul Makonda amekabidhiwa Magodoro hayo Mjini Dodoma na Kiwanda hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mhe. Makonda amepiga marufuku kitendo cha Wagonjwa kulazwa chini Hospitalini kwa kuwa Magodoro hayo yanaenda kutatua kero hiyo.

Amesema kuwa Magodoro aliyopatiwa atayakabidhi kwenye Hospital zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa baadhi zimekuwa na upungufu wa Magodoro hali inayofanya Wagonjwa kulala juu ya Vyuma vya kitanda na wengine kutandika Kanga na Nguo kwenye sakafu.

Amesema idadi kubwa ya Wananchi wamekuwa wakitoka Mikoani kufuata huduma za Afya Dar es Salaam kutokana na wingi wa Hospital za Kisasa za Umma na Binafsi hivyo kusababisha Hospital kuwa na Wagonjwa wengi.

Licha ya Changamoto hiyo Mhe. Makonda amesema Sekta ya Afya Jijini Dar es Salaam imeimarika kwa kiasi kikubwa ambapo lengo lake ni kuona Mkoa huo unakuwa kinara kwenye utoaji wa huduma Bora za Afya.

Ameshukuru kiwanda hicho na Wadau waliomuunga Mkono na kuwasihi wananchi kununua Magodoro ya Dodoma Asili yanayotengenezwa na Kiwanda cha Wazawa ili kukuza Uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Jordan Rugimbana amempongeza RC Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya katika Sekta mbalimbali ikiwemo Maboresho ya Jeshi la Polisi na kusema ataenda Dar es salaam kujifunza namna walivyofanikiwa kwenye Ulinzi na Usalama.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda cha Magodoro ya Dodoma Asili Bwana Haider Gulamali amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa RC Makonda kwakuwa kazi anayoifanya ni kubwa na inawagusa Wananchi wote hususani wanyonge.

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Operesheni Panya Road Imekuwa na Mafanikio

    May 27, 2022
  • RC Makalla Asimamisha Shughuli za Uchimbaji Madini Boko - DSM

    May 26, 2022
  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa