• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makonda Akabidhi Mabasi 4 Yaliyokuwa Mkweche kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Posted on: November 2nd, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 4 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mabasi 4 aliyoyakabidhi RC Makonda Leo ni Kati ya Mabasi 11 yaliyokuwa yamekufa (mkweche) ambapo baada ya RC Makonda kuyaona na kubaini uhaba wa magari kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliwatafuta wafadhili wa Kampuni ya Dar Coach Ltd waliojitolea kuyarejeshea uhai magari hayo na hatimae leo yanatembea Barabarani yakiwa mazima.

RC Makonda amesema ukarabati wa mabasi hayo ulihusisha Kubadilisha Bodi, kupaka Rangi, kubadili Viti, kuweka Mfumo wa kuchaji simu, AC, TV, Taa,Madirisha, Matairi pamoja na kuongeza na kupunguza idadi ya viti.

Aidha RC Makonda amesema mkakati wa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama utaendelea ikiwa ni pamoja na kugusa maisha ya mtumishi mmojammoja kwa kuwapatia mikopo ya viwanja vya bei nafuu.

Hata hivyo RC Makonda ameshukuru Kampuni ya Dar Coach Tanzania Ltd kwa uzalendo walioonyeaha kukarabati magari hayo pasipo kutumia pesa ya serikali.

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amempongeza RC Makonda kwa ubunifu wa kufufua magari yaliyokuwa yamekufa ambapo ameeleza kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea ufanisi katika kazi kwa kupunguza changamoto ya usafiri.

Mabasi 4 yaliyokabidhiwa leo ni Ashok Leyland 01, Iveco 2 na Toyota Coaster moja huku magari mengine 7 yakiwa hatua ya mwisho kukamilika.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • RAS MADENGE ASISITIZA UTOAJI HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI

    January 24, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa