• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Operesheni ya Panya Road DSM ni Endelevu

Posted on: September 13th, 2022

 

-Asema DSM ni Salama awataka Viongozi wa Serikali za Mitaa kuhamasisha Ulinzi Shirikishi

-Aagiza Watuhumiwa wa Ujambazi na Panya road Wanaotoka Magerezani kufuatiliwa

-Apongeza wananchi Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Mzinga

RC Makalla ameyasema hayo leo Septemba 13,2022 alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha kisasa cha Polisi katika Kata ya Mzinga- Mwanagati Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

RC Makalla amesema Operesheni ya Panya road ni endelevu wananchi wasiwe na hofu waendelee kufanya shughuli zao za kujiletea kipato kwa kuwa Dar es Salaam ni Salama kabisa, amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa kuhamasisha Ulinzi Shirikishi Katika maeneo yao.

Aidha RC Makalla ameelekeza Magereza yote DSM kuhakikisha Watuhumiwa wa Ujambazi na Panya road Wanapotoka Magerezani taarifa na majina yao ipelekwe kwa OCD au RPC ili kuweza kufuatilia mienendo yao wanapokuwa uraiani

Sambamba na hilo Mhe Makalla amepongeza ushiriki wa wanachi katika Ujenzi wa Kituo cha Polisi ambapo amesema amejifunza wananchi wakishirikishwa wanaweza kituo hicho ni cha kisasa, cha mfano wananchi maeneo mengine waige mfano huo.

Mradi wa Kituo hicho cha Polisi Mwanagati kukamilika kwake kutagharimu Tsh Milioni 211,964,400 mpaka kituo kilipofikia sasa tayari kimegharimu Tsh Milioni 151,534,400 kati ya hizo shilingi milioni 45,000,000 ni mchango wa Halmashauri, milioni 96,334,400 mchango wa Wananchi na shilingi milioni 10,200,000 mchango wa Serikali Kuu ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Hata hivyo RC Makalla amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kupata kiasi cha milioni 60 ambacho kinahitajika kukamilisha Ujenzi wa Kituo, huku  akiagiza kufikia ijumaa awe kupatiwa BOQ ili kujua vifaa vinavyohitajika kwa ili Ofisi yake iweze kusaidia kupitia Wadau wa maendeleo.

Mwisho RC Makalla amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua msingi mkubwa wa maendeleo katika Jamii ni Utulivu ambao unatokana na Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao hivyo DSM ni Salama Serikali ya Mkoa iko makini kusimamia jambo hilo bila kuchoka muda wote usiku na mchana

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa