• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla- Serikali yenu ni Sikivu, Kesho Tunaendelea na Chanjo ya Uviko-19 Hapa.

Posted on: August 22nd, 2021

-Amuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa kuendelea kutoa huduma kesho Agosti 23, 2021 katika uwanja wa Uhuru

-Awaagiza wakuu wa Wilaya katika maeneo yao kuendeleza utaratibu wa kutenga maeneo ya wazi kuwapatia chanjo wananchi

-Asisitiza amekuwa akiendelea  kupokea maombi mengi kutoka makundi anuai kama Bodaboda, Bajaji, madereva wa magari makubwa na wengine wengi

Mhe Amos Makalla akishuhudia mmoja kati ya maelfu walijitokeza kupata chanjo ya UVIKO - 19 uwanja wa Uhuru mapema leo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ametembelea viwanja vya Uhuru Temeke  kujionea mwenendo wa utoaji chanjo ya UVIKO-19 kufuatia tamko lake kwa umma la kutoa huduma hiyo kwa uwazi siku ya Jumapili Agosti 22, 2021 ambayo ni leo.

Mhe Makalla akipita kukagua namna zoezi la chanjo ya UVIKO-19 linavyoendelea katika Uwanja wa Uhuru.


Akiwa katika uwanja wa Uhuru  Mhe Makalla amejionea muitikio mkubwa na kumlazimu kumuagiza Mganga Mkuu Mkoa Dkt Rashid Mfaume kuendelea na huduma hiyo uwanjani hapo kesho.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa amesema nimekuwa nikiendelea kupokea maombi mengi kutoka makundi mbalimbali na hiyo inatokana na zoezi hilo kuendeshwa kwa kuangalia makundi maalum hususani watu wenye zaidi ya miaka 50 na wale walioko katika mazingira hatarishi.

Hivyo wale wa miaka 18 na kuendelea kuikosa fursa hiyo ndio maana Mkoa ukaona kuna kila sababu ya kutenga siku na sehemu ya wazi ili wananchi wapate huduma hiyo kwa urahisi.

"Zoezi hili limefanikiwa kama mnavyo ona, niwashukuru wananchi wanaoendelea kupata chanjo nitoe rai msiwe na wasiwasi hata mimi Mkuu wenu wa Mkoa na Katibu Tawala hapa nimeshachanja na niko vizurii.. safiii kabisa" Alisema Mhe Makalla

Aidha amewaagiza wakuu wa Wilaya katika maeneo yao kuendelea na huduma hiyo kwa kutenga maeneo ya wazi ili wale wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wapate chanjo.

Vilevile Mhe Makalla amesema katika uwanja huo wa Uhuru  watu 100 hupata huduma ya chanjo kwa wakati mmoja na kwa taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa Mkoa takwimu za waliochanja ukiunganisha na wa siku ya leo hadi kufikia saa 4 asubuhi ni zaidi ya watu 2882

Chanjo hii ni bora, Salama, na yenye Ufanisi Mzuri










 





Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa