• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKALLA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUTOA FEDHA UJENZI WA MADARASA 618

Posted on: October 7th, 2022

-Asema Mkoa umepokea Bilioni 12 na milioni 360 kwa ajili ya Ujenzi huo
- Aelekeza Ujenzi wa vyumba vya madarasa ufanyike kwa Force Account
- Ataka  Ujenzi kuzingatia Ubora, thamani ya pesa na kukamilika kwa wakati
RC Makalla amesema hayo leo Octoba 7,2022 katika kikao chake na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari DSM, Ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja, ambacho kilihudhuliwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Elimu, na Sekretarieti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge
Mhe Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kufuatia Mkoa huo kupewa kiasi cha Bilioni 12 na milioni 360 ambazo zimeelekezwa katika Ujenzi wa vyumba vya  madarasa 618 sawa na shule 108
Aidha RC Makalla ameelekeza kujenga Madarasa ya mfano kwa kutumia Force Account huku akisisitiza pesa hizo zikatumike kujenga madarasa na sio kulipa fidia.
Vilevile Mhe Makalla amewataka kusimamia vizuri zoezi hilo kwa kuzingatia thamani ya pesa na Ubora bila kusahau kazi ifanyike kwa wakati ifikapo Novemba 30,2022 Ujenzi uwe umekamilika.
Sambamba na hilo RC Makalla amesema amepokea migogoro 41shule za Sekondari na 25 Shule za msingi ya uvamizi wa Ardhi maeneo ya shule hivyo amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwenda kumaliza migogoro hiyo kwa kuyatembelea maeneo hayo, kuyakagua, Kuyajua vizuri maeneo hayo na kuweka mipaka
RC Makalla ameelekeza migogoro yote ikashughulikiwe kwa ufanisi na apatiwe taarifa ya Utekelezaji wa zoezi hilo
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Gondwe kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wengine amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwenda kutekeleza maagizo yake aliyotoa ili ifikapo Januari 2023 wanafunzi waingie katika vyumba hivyo vya madarasa

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Ataka DSM ya Kijani na Bustani za Watu Kupumzika

    March 25, 2023
  • RC MAKALLA AFUNGUA SEMINA YA USAMBAZAJI NA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 DSM

    March 24, 2023
  • RC MAKALLA AFUNGUA MKUTANO WA "AFRICA E- MOBILITY FORUM"

    March 21, 2023
  • RC Makalla Akabidhi Hundi ya Mikopo ya 10% zaidi ya Bilioni 4.6 Temeke Atoa Maagizo Matano

    March 20, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akikagua Maendeleo ya Ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa