• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Aipongeza Benk ya NMB kwa Kubuni Huduma Rafiki kwa Wananchi Wote

Posted on: June 21st, 2022

 

Baadhi ya Wataalam wa NMB wakifuatilia kwa makini wakati wa Semina ya NMB kwa waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Mkoa wa DSM katika ukumbi wa Kamrimjee Ilala -Dar es Salaam


- Awahimiza kuendelea kubuni huduma nyingi na rafiki kwa Makundi yote kwenye Jamii.

- Awapongeza kwa kutoa Gawio la Shilingi Bilioni 30.7 kwa Serikali.

- Awashukuru kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa Katika matukio mbalimbali ya kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Bank ya NMB kuendelea kubuni huduma rafiki kwa Makundi mbalimbali katika Jamii ili kuweza kuwafikia Wateja wengi Zaidi.

RC Makalla ametoa wito huo wakati wa Warsha kwa Viongozi wa Serikali wa Mkoa huo iliyolenga kueleza Fursa mbalimbali zinazopatikana katika bank hiyo ikiwemo mikopo ya riba nafuu.

Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Halmashauri za Mkoa huo kushirikiana na Bank hiyo hususani kwenye kukopa fedha za kuwezesha kutekeleza miradi yenye Tija na itakayoongeza mapato kwa Halmashauri.

Aidha RC Makalla amepongeza Bank hiyo kwa kutoa Gawio la Shilingi Bilioni 30.7 kwa Serikali pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoonyesha kwa Serikali ya Mkoa huo katika kufanikisha masuala ya kijamii ikiwemo Elimu, Afya, Usafi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Bank hiyo Ruth Zaipuna amesema malengo matano ya kuandaa Warsha hiyo ni pamoja na kuwaeleza faida ya kutumia bank ya NMB, Uwezo wa Bank na utayari wa kufanya Kazi nao, Kutumia Fursa ya Teknolojia na ubunifu wa bank yao katika ukusanyaji mapato na Malipo mbalimbali.

Aidha Zaipuna amesema lengo Lingine ni kuomba Halmashauri kushirikiana na Bank katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mikopo ya riba nafuu na Kuwaomba Viongozi hao kuwa mabalozi kwenye kutambulisha bidhaa zao.

Bi. Zaipuna pia amemuhakikishia RC Makalla kuwa bank ya NMB itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo katika masuala yote ya kijamii

Mtendaji Mkuu wa Benk ya NMB Ruth Zaipuna akitoa taarifa ya lengo la Benk hiyo kufanya semina kwa Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Mkoa huo katika ukumbi wa Karimjee.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa