• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Afunga Mafunzo ya 14 Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) kwa niaba ya Waziri wa OR-TAMISEMI

Posted on: February 10th, 2023

 


-Asema Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe Angellah Kairuki anawapongeza kwa Moyo, Uzalendo na mchango wa NDC kwa Taifa

-Ahadi ya Mhe Waziri Kairuki Serikali itaendelea kuwaleta Viongozi wengi zaidi kupata mafunzo NDC

- RC Makalla awataka Viongozi waliopata mafunzo kutumia katika kutatua migogoro ya wananchi

CPA Amos Makalla kulia akiwa katika picha na Mkuu wa Chuo NDC Meja Jenerali Michael Mhona baada ya kuwasili chuoni hapo


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Februari 10, 2023 amefunga mafunzo ya 14 katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) yaliyohusisha Viongozi wa mhimili wa Dola, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, na Viongozi waandamizi kutoka kwenye Wizara

CPA Makalla wakati akifunga mafunzo hayo amesema amekuja kwa niaba ya Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe Angellah Kairuki ambaye ameshindwa kuja kutokana na sababu zisizo zuilika, ambapo amesema Mhe Waziri anakipongeza NDC kwa Moyo, Uzalendo, na mchango wake kwa Taifa katika kutoa mafunzo Usalama wa Taifa na Stratejia kwa Viongozi mbalimbali hapa nchini.

Aidha CPA Makalla amebainisha katika hotuba ya Waziri wa OR-TAMISEMI ahadi yake ni kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na chuo hicho kwa kuleta Viongozi wengi zaidi kwa masilahi mapana ya Taifa

Hata hivyo CPA Makalla amewataka Viongozi waliopata mafunzo katika chuo hicho kutumia maarifa waliyopewa *kutatua migogoro ya wananchi katika maeneo yao*, wananchi wanachanga moto nyingi na wanaimani kubwa na Viongozi hususani wateule wa Rais.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenelari  Ibrahim Michael Mhona amesema mafunzo waliyopatiwa Viongozi takribani 114 yakiongozwa na kauli Mbiu " Uongozi wa Kimkakati kwa Mazingira Yanayobadika kiusalama Tanzania" wameyapata kwa asilimia mia moja, malengo ya kozi yamefikiwa wajibu wao ni kwenda kuyafanyia kazi yale waliyojifunza kwa muda wa siku 5 kwa lengo la kuleta Ustawi wa Jamii na Taifa kwa Ujumla.

Mafunzo hayo ni ya 14 ambapo wahitimu wapatao 114 wamehitimu, ni mafunzo ya muda mfupi ambayo Viongozi wameyapata kwa siku 5 kuanzia  Februari 06, 2023 hadi leo ebruari 10,2023  katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania- Kunduchi Wilaya ya Kinondoni

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa