• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Makalla Aagiza Shule zote DSM Kushiriki Kufanya Usafi na Kupanda Miti katika Maeneo Yao

Posted on: January 28th, 2022

 

RC Makalla akikabidhi vifaa vya Usafi kwa Walimu mapema leo katika viwanja vya shule ya Msingi Zanaki Ilala DSM.

- Awaomba wananchi Kesho Jumamosi kushiriki usafi wa pamoja

- Agawa Vifaa vya Usafi kwa Shule zote za Sekondari na Msingi DSM

- Apongeza Zanaki Sekondari kuwa Mabalozi wazuri wa Usafi

-Ataka Maafisa Elimu kutoa Maelekezo au waraka katika kila Shule kufanya usafi na  kupanda miti

- NMB waahidi kuunga Mkono Kampeni za RC Makalla

- Wanafunzi washukuru na kuahidi kuendeleza Usafi DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo Januari 28, 2022 amegawa Vifaa vya Usafi kwa shule za msingi na Sekondari DSM katika Viwanja vya shule ya msingi Zanaki Ilala-Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM.

RC Makalla ameyasema hayo leo  katika Shule ya Sekondari ya Zanaki wakati akipokea Vifaa vya Usafi kutoka Benki ya NMB na kuvigawa katika Shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo Dar es Salaam

Hata hivyo  Mkuu wa Mkoa ameipongeza Shule ya Zanaki Sekondari kwa kuwa Mabalozi wazuri wa Usafi ambapo amesema Mazingira yao ni mazuri Sana na kuwataka kuendelea kuboresha Bustani na kupanda miti

Wakati huo huo RC Makalla amewataka  Maafisa Elimu kutoa Maelekezo kwa Shule zote kuanza Kampeni za Usafi wa Mazingira, upandaji wa miti na kuanzishwa kwa Mabustani*

Kwa upande wa NMB, Meneja wa Kanda ya Dsm Bwana  Donatus Richard ameahidi kuendelea kuunga Mkono juhudi zote za  RC Makalla

Nao Wanafunzi wa Zanaki wamesema wanamshukuru Sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuahidi kuendeleza Usafi majumbani na shuleni

Ikumbukwe kuwa Kampeni ya Usafi ulizinduliwa na Mhe. Amos Makalla tarehe 4 Desemba 2021 na kupokelewa vema na Wananchi wa Dar es Salaam

RC Makalla ametoa RAI kwa wakazi wa Dar es Salaam kushiriki Siku ya Kesho tarehe 29/01/2022 kufanya usafi wa pamoja katika maeneo yao, yeye ataungana na wakazi wa Manzese Manispaa ya Ubungo kufanya usafi wa pamoja

SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa