• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Azindua Harambee Kabambe ya Kuchangia zaidi ya Bilioni 3 Hospitali ya Amana

Posted on: July 5th, 2024

 

 

-Asema upatikanaji wa fedha hizo utawezesha upanuzi na ukarabati wa majengo ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa

-Atoa rai kwa wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia

-Abainisha kilele cha Harambee hiyo ni Agosti 31,2024 katika ukumbi wa Mlimani City

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albaert Chalamila leo Julai 05,2024 amezindua harambee kabambe ya kuchangia upanuzi na ukarabati wa majengo ya hospitali ya Rufaa ya Amana, ambapo harambee hiyo inalenga kukusanya zaidi ya bilioni 3.

Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika katika viunga vya Hospital ya Amana RC Chalamila amemshukukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa ambao ameufanya na anaendelea kufanya katika sekta ya Afya hapa nchini hususani Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo kupitia juhudi hizo ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kuunga mkono juhudi za Mhe Rais kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii.

Aidha RC Chalamila amesema kwa sasa itafanyika harambee yenye lengo la kukusanya zaidi ya bilioni tatu kuwezesha ukarabati na upanuzi wa majengo ambayo yapo  na yatabeba huduma nyingine wakati tutakapoanza kubomoa baadhi ya majengo yatakayo bomolewa kupisha mradi huo mkubwa na wa kihistoria ikiwa ni kuendeleza kuunga mkono juhudi za Mhe Rais “Leo Julai 05,2024 ni uzinduzi rasmi na kilele chake ni Agosti 31,2024 katika ukumbi wa mlimani City mgeni rasmi anatarajiwa kuwa kiongozi wa kitaifa ambapo taarifa rasmi itatolewa hivyo tuendelee kujipanga vizuri kwa ajili ya siku hiyo” Alisema RC Chalamila.

Kwa Upande wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt Kiwelu amesema unaweza kuona kwa sasa majengo yako mithili ya kijiji cha ujamaa na mpango mpya yako machache na yaliyopangwa kwa hekima.  Hivyo kupitia harambee hiyo jengo jipya la huduma za mama na mtoto ambalo litajengwa Amana litakuwa lenye vitanda zaidi ya 350 pia jengo la Utawala la kisasa ambapo utofauti katika jengo la utawala ni kuwa kutakuwa na makumbusho (Museum) ambayo itakusanya historia nzima ya Afya nchini Tanzania. 

Vilevile Jengo hilo litakuwa na maabara za kisasa za kujifunzia kwa vitendo (clinical skills laboratories), madarasa, kumbi za mikutano, ofisi, kutakuwa na huduma za kibenki, maduka ya vifaa tiba, supermarket, hoteli na zaidi kutakuwa na ukuta wa dhahabu ambapo majina ya wote watakaochangia hospitali hii yatatunzwa kama kumbukumbu ya vizazi vijavyo kudhihirisha nguvu ya umoja wetu.  “Hatutaki maisha ya kuishi kwa nadharia tunataka kuwarahisishia maisha watoto wetu kujua historia ya sekta ya Afya ndani ya muda mfupi wafikapo Amana” Alisema Dkt Kiwelu.  

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa