• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Atangaza Ujio wa Wakuu wa Nchi Mbalimbali DSM

Posted on: July 21st, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 21, 2023 ametoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari ujio wa wakuu wa nchi mbalimbali kwenye mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu rasilimali watu utakaofanyika tarehe 25-26 kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere- JNICC Dar es Salaam.

RC Chalamila amesema Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndio mwenyeji wa mkutano huo mkubwa ambapo wakuu wa nchi za Bara la Afrika kuja na Azimio la kujenga Afrika mpya yenye kuzingatia mahitaji ya Rasilimali watu kama ilivyo kuwa Falsafa ya Rais wa kwanza wa Taifa hili Mwl JK Nyerere alisema " ili tuweze kendelea tunahitaji vitu vinne Watu , Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora " watu wenye ujuzi na weledi, Azimio la Dar es Salaam lina kwenda kujenga na kutathimini mambo ya kuzingatia ili kufikia mwongozo wa Bara la Afrika lenye watu wenye thamani ya kuendeleza Bara hili.

Adha RC Chalamila amesistiza kuwa Ugeni huu ni Jiji la Dar es Salaam Jiji la maraha ambalo Afrika inalitumia katika kuhakikisha Azimio juu ya ufanyaji kazi wa kizazi cha Afrika unaimarika kwa manufaa ya Bara la Afrika, Tanzania ni nchi ya mfano kwenye mambo mengi hivyo hatuna budi kumshukuru *Rais Dkt Samia Suluhu Hassan* kwa jitihada yake katika kukuza uchumi na kujenga taswira nzuri ya nchi yetu ndani na nje ya nchi.

Vilevile ni ukweli usiopingika toka Rais Dkt Samia aingie madarakani amewekeza nguvu kubwa kujenga taswira nzuri ya nchi na matunda yake ndio haya tunaona ya kufanyika kwa mkutano mkubwa wa wakuu wa nchi Bara la Afrika kuhusu Rasilimali watu.

Mhe Chalamila amesema Mikutano hii ni Sehemu ya Utalii na ujio wa wageni ni muhimu katika kujenga utalii wa mahoteli, fukwe na vyakula vya Kitanzania, kutakuwa na wageni wasiopungua 1,200 watakao lala, kula vyakula na kutembelea maeneo mbalimbali hivyo tuitumie vizuri fursa hii.

Hata hivyo Mhe Albert Chalamila amesema lengo kuu la Serikali ya Mkoa ni kuhakikisha wageni wanaacha Dola hapa hivyo tumeanda maeneo maalum ambayo wafanyabishara na wajasiriamali wataweka bidhaa zao kwa ajili ya kuuza katika eneo la nje la Ukumbi wa JNCC

Sambamba na hilo Mhe Chalamila amewataka wakazi wa Jiji hilo kuendelea kuliweka Jiji safi, pia ameeleza sababu ya Benki ya Dunia kuridhia mkutano huo mkubwa kufanyika Tanzania- Dar es Salaam ni kutokana na Amani iliyoko, kuwepo kwa vijana wengi wasio na ajira kama ilivyo kwa nchi nyingine za Africa hivyo watajifunza namna nchi inavyokabiliana na Changamoto na Utaoji wa elimu bila malipo kwa Shule za msingi na Sekondari kama mkakati wa kuzalisha wataalam nalo watajifunza.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Ndg Ephraim Mafuru amesema hadi kufikia leo Julai 21, 2023 maandalizi yote muhimu yamekamilika katika nyanja zote kumbi na vifaa vyote muhimu viko tayari

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa