• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aagiza Kuundwa kwa Kamati ya Kuchunguza Mwenendo wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti

Posted on: December 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametoa maagizo hayo leo Desemba 22, 2023 wakati wa ziara yake ya kukagua machinjio hayo yanayojengwa kwa thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 19 ambapo hadi sasa yamekamilika kwa asiliamia 97.

RC Chalamila alisema machinjio hayo yaliyoanza kujengwa tangu 2019 ni ya kisasa  yenye uwezo wa kuchinja ngo'mbe elfu moja kwa siku na ikiwa ng'ombe mmoja akachinjwa kwa sh 20,000 serikali itapata mapato yatakayosaidia kuendesha gharama za uendeshaji ambazo ni kubwa kutokana na mitambo yote inayotumika inatumia umeme tu.

Pia RC Chalamila alikemea vitendo vya rushwa kwa watumishi vilivyobainishwa na wafanyabiashara hao hivyo aliagiza kamati iundwe itakayochunguza mwenendo na uadilifu wa watumishi.

"Na baada ya kukamilika kwa  kamati hiyo ndogo ambayo itakuwa na watu mbalimbali, wakiwemo watu wa usalama, watu wa TAKUKURU, watu wa utumishi wa umma, wahandisi na wengine itatupatia majawabu ya miundombinu ya namna ya uchinjaji na mchakato wote," alisema RC Chalamila.

Aliendelea, "Nitoe rai kwa watu wanaohusika na ujenzi huu hasa kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wahakikishe wanakamilisha ujenzi huo na kufunga vifao vyao haraka iwezekanavyo ili Rais Samia Suluhu Hassan atakavyotembelea hapa kwa ajili ya kuzindua au kufanya mengine kusiwe kuna dosari ya aina yoyote."

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo alitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa kwa kufanya ziara na kuahidi yote waliyoagizwa wataenda kuyafanyia kazi zikiwemo changamoto zilizosababisha mradi huo kutokukamilika kwa wakati.

Awali mwenyekiti wa wafanyabiashara machinjioni hapo, Emanuel Siliake alimueleza RC kuwa kuna baadhi ya watumishi wamekuwa na utendaji mbaya, vitendo vya rushwa na kuchukua nyama zao kwa kutumia nguvu na kutusababishia wao kupata hasara.

Pia RC Chalamila alifika katika viwanja vya msikate tamaa vilivyopo kata ya Vingunguti na kushiriki zoezi la utoaji wa vitambulisho vya NIDA kwa wananchi, na aliwasihi wananchi wakachuke vitambulisho vyao kwakuwa baada ya mwezi mmoja kupita wataenda kuvichukua kwa pesa kama gharama yakuhifadhiwa kwa mkoa wa DSM, Sambamba na hilo aliwaambia wananchi washerehekee sikukuu kwa amani sababu ulinzi upo Mkoa umejipanga vizuri.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa