• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RAS Dkt Toba Nguvila Ahamasisha Wananchi Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Posted on: November 23rd, 2024

 

-Aongoza Bonanza la kuhamasisha jamii kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27,2024

-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuendelea kulinda amani ambayo ni Tunu ya Taifa.

Katibu wa Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt  Toba Nguvila ameongoza mamia ya wakazi wa Mkoa huo katika  Bonanza la kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Akitoa hotuba wakati wa Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Katibu Tawala wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo na na kulinda Amani ambayo ni Tunu ya Taifa kwa umahiri mkubwa ambapo alisemaBonanza hili, limehusisha michezo ya aina mbalimbali ikiwemo matembezi ya Polepole ambayo yalianzia Uwanja wa Uhuru hadi Mwembe Yanga Pia Michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, mchezo wa kuvuta Kamba na mingine mingi.

Aidha Dkt Toba alisema Kupitia Bonanza hili viongozi wa Serikali,vyama vya Siasa wamepata fursa ya kujumuika na wananchi mbalimbali wa Mkoa, kubadilishana mawazo pia kujadili masuala yanayohusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na umuhimu wa kushiriki katika  uchaguzi huo.

Sanjari na hilo imekuwa fursa adhimu kwa kila mmoja aliyeshiriki Bonanza hili ambapo wananchi wamejipatia  elimu kuhusu haki zao za kisheria na ushiriki wao katika uchaguzi wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi wenye uwezo wa kusimamia maendeleo na kuunganisha jamii zao.

Vilevile Dkt Toba alisema Ofisi ya Rais -TAMISEMI inaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni sehemu muhimu ya kukuza demokrasia na maendeleo katika jamii,na hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashiriki kupiga kura kwa wingi na kwa Amani.

Mwisho Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Nguvila alikabidhi tuzo na zawadi mbalimbali kwa washindi wa Bonanza hilo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi,Jitokeze Kushiriki Uchaguzi

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa