• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Rais Samia Aruhusu Kurudishwa Wafanyabiashara Soko la Karume

Posted on: January 24th, 2022

 

# Asisitiza Waratibiwe sio kurudi  Kiholela

# Asema Watajenga Wenyewe kwa Ghalama zao

#Wafanyabiashara( Wamachinga) watakiwa kutoa Ushirikiano kwa DC, MD na Wataalamu husika

#Wafanyabiashara ( Wamachinga) Wamshukuru Rais   Samia,  RC. Makalla na DC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Wafanyabiashara( wamachinga) wa Soko la Karume (Mchikichini) kurudishwa Mara moja katika eneo lao la Biashara soko la Karume

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mh. Amos Makalla leo tarehe 24 Januari 2022 katika Mkutano wake na wafanyabaishara (Wamachinga ) uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Karume ( TFF)

Mhe. Makalla amesema kuwa Rais Samia amesisitiza Wafanyabiashara hao (Wamachinga) waratibiwe vema na uongozi husika na sio kurudi Kiholela

Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema Rais ameelekeza kuwa  Wafanyabiashara hao (Wamachinga) Watajenga Wenyewe kwa Ghalama zao lakini wataelekezwa vema (wataratibiwa) na Wataalamu ambapo itapatikana njia ya kuingia na kutoka

Mhe. Makalla ameongeza kuwa Wafanyabiashara hao (Wamachinga) wametakiwa kutoa Ushirikiano kwa Mkuu wa Wilaya Ilala, Mkurugenzi, Wataalamu na Kamati husika

Kwa upande wa Wafanyabiashara (Wamachinga) Wamemshukuru *Rais Samia Suluhu Hassan* *Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam* na *Mkuu wa Wilaya ya Ilala* na *Uongozi wake* kwa kuwarejesha katika maeneo yao ya Biashara na kuahidi kutoa Ushirikiano katika Serikali mwanzo mwisho

Ikumbukwe kuwa Leo tarehe 24 Januari 2022 *Mhe. Makalla* amepokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi ya Uunguaji wa Soko hilo la Karume ambapo Kamati imebaini kuwa Chanzo Cha moto huo ni kutokana na *Mshumaa* ambao uliwashwa na kijana anayesadikika kutumia madawa ya kulevya kisha akasinzia.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa