• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

"Nimedhamiria Kuboresha Fukwe Zote Dar, Kwa ajili ya Utalii na Mapumziko, Naanza na Coco Beach" RC Makalla

Posted on: August 24th, 2021

  

Mhe Makalla akikagua eneo la Coco beach mara alipozuru katika fukwe hiyo.


- Amesema hatuwezi kuwa na fukwe ukikaa unaziba pua, fukwe ziwe safi zivutie

- Aagiza kuwaorodhesha wafanyabiashara wote waliojenga vibanda eneo la Coco mara moja na zoezi liishe leo

- Awaalika Wadau kama NMB, PEPSI, TBL, COCA na wengine wengi kumsaidia kutimiza dhamira yake

- Amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuleta umeme wa uhakika katika eneo la Coco beach mara moja

- Atangaza neema kwa wafanyabishara wadogowadogo katika eneo hilo awataka kujiunga katika vikundi ili watumie fursa za mikopo ya 10%

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 24, 2021 amezuru eneo la Coco beach Kinondoni, Dar es Salaam.

Akiwa katika eneo hilo pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Kigamboni alipata wasaa  wa kulizungukia eneo hilo na kuongea na wafanyabiashara wenye vibanda mahali hapo.

Mhe Makalla amebainisha dhamira yake ya kuboresha fukwe zote za Dar es Salaam  na maeneo ya wazi, kwa kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote, ziwe ni beach zinazovutia utalii na sehemu nzuri za mapumziko.

Kwa hatua za awali Mhe Makalla ameagiza mara moja kuanza kwa zoezi la kuwaorodhesha wafanyabiashara wa eneo hilo na zoezi liishe leo Agosti 24, 2021 pia amewataka kuondoa hofu hakuna atakayenyang'anywa eneo bali kinachofanyika ni maboresho ili eneo hilo liwe kivutio cha Utalii na watu kupumzika.

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema anawaalika wadau kama NMB, PEPSI, TBL, COCA na wengine kuunga mkono juhudi za Serikali na dhamira yake ya kuziendeleza fukwe hizo kwa maslahi Mapana ya Mkoa na Taifa.

Sambamba na hilo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Godwin Gondwe kuleta umeme Coco beach na kujenga ofisi ambayo watumishi wachache watutumia wakati wakiwa wanasimamia fukwe hiyo.

Mkuu wa Mkoa Pia ametangaza neema kwa wafanyabishara wadogowadogo wa eneo hilo kwa kuwataka kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo ya 10% inayotolewa katika Manispaa, amesisitiza kuanzia sasa vibaka hawana nafasi amuagiza kamanda wa Polisi Kinondoni kusimamia hilo.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa