• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM

Posted on: August 24th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa  Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Mhe. Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.

Mhe. Makonda amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Joseph Pombe Magufuli ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.

Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.

Aidha Mhe.Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo kutajengwa Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Banki ya Dunia na Serikali ya Japan.

Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.

Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa