• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge Atembelea Miradi Katika Jiji hilo

Posted on: August 5th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 5 Agosti , 2020.

Awali alianza kutembelea  mradi wa machinjio ya kisasa iliyopo Vingunguti katika Manispaa ya Ilala ambako alishuhudia ujenzi unavyoendelea wa machinjio hiyo ulioenda sambamba na uwepo wa vifaa vya kisasa ambavyo vitafungwa kwa ajili ya kutekeleza zoezi zima la uchinjaji wa nyama ili kuwapatia huduma bora wananchi.


Akiwa katika machinjio hiyo alipokea taarifa ya ujenzi huo unavyoendelea na kupongeza zoezi zima linavyoendelea na kueleza kuwa tarehe 30 Septemba,2020 machinjio hiyo iwe imekamilika.

Mhe. Mkuu wa Mkoa Abubakar aliomba wananchi kusaidiwa ili kujua masoko ya kuuzia nyama zao sambamba na uwepo wa huduma zote za msingi kama katika eneo hilo kama vile maji, umeme na barabara nzuri.

Baada ya kutoka katika machinjio ya kisasa ya Vingunguti  Mkuu wa Mkoa alielekea katika Ujenzi wa soko la Kisutu ambapo alikagua mradi huo na kupokea taarifa kutoka kwa msimamizi wa mradi huo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa Abubakar alisema haridhishwi na hali ya ujenzi wa soko la Kisutu kwani mradi huo ulipangwa kukamilika Agosti 24,2020 lakini mpaka sasa umekamilika kwa asilimia sitini tu hivyo alitoa miezi miwili tu kwa Mkandarasi kumaliza mradi huo badala ya miezi sita aliyoomba kuongezewa mkandarasi huyo.

Baada ya hapo msafara wa Mhe. Mkuu wa Mkoa ulielekea katika jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambapo hapo alipokea taarifa kutoka kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya wa Manispaa hiyo ambapo alieleza kuwa utekelezwaji wa mradi huo umekua ukisua sua kwani mpaka sasa TBA ambao ndio wajenzi wa jengo hilo mkataba wao uliisha tangu tarehe 22 Juni,2020 na ujenzi umefikia asilimia sabini na tano tu.

Alieleza kuwa, watumishi wa manispaa hiyo wamekuwa wakifanya kazi kwa tabu sana kwani wako katika maeneo mbalimbali sambamba na Manispaa hiyo kuingia hasara ya kulipa pango katika maeneo ambayo watumishi hao wamepanga.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa Abubakar alimpatia mkandarasi wa mradi huo Wiki sita tu ili akamilishe mradi huo. Alimtaka mkandarasi wa mradi huo kuweka wafanyakazi wa kutosha sambamba na kufanya kazi usiku na mchana.

Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa Abubakar iliishia katika mradi wa stendi ya Mbezi luis ambapo alitembelea na kujionea hali halisi ya mradi huo kisha kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ambapo alimpongeza Mkurugenzi huyo na Timu yake kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa mradi huo mpaka kufikia hatua iliyopo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa Abubakar alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kukamilisha mradi huo ndani ya wakati uliopangwa na kushauri kuwa mradi huo unapokamilika watu wa kuingia wawe wameshapatikana sambamba na kuwepo kwa utaratibu mzuri wa uendeshaji wa mradi huo mkubwa.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa