• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

MHE. PAUL MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM

Posted on: August 25th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwa ajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.

Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwa ajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

Mhe. Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200, Kompyuta 100, Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

Aidha Mhe. Makonda amemuagiza aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa matano.

Agizo hilo limekuja baada ya hivi karibuni Msamaria mwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa Dawa za kulevya kwenye moja ya Hotel na Askari walipofika kwenye Hotel hiyo wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda Mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel kisha kufanya fujo kumtafuta aliyetoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabaini Askari hao.

Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa na Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze Picha hizo kitendo ambacho ni kinyume na Sheria ambapo Mheshimiwa  Makonda amesema hawezi kuruhusu vitendo kama hivyo vitendeke kwenye Mkoa wake na kuongeza kuwa  anataka kuona Sheria na Haki vinatendeka kwa Wananchi.

Mhe. Makonda pia amebaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanaowabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Operesheni Panya Road Imekuwa na Mafanikio

    May 27, 2022
  • RC Makalla Asimamisha Shughuli za Uchimbaji Madini Boko - DSM

    May 26, 2022
  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa