• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC MAKONDA: NIMEDHAMIRIA KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU

Posted on: August 1st, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ameelezea Dhamira yake ya kuhakikisha ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za walimu pamoja na Vyoo kwa shule za Msingi na Sekondari zilizobainika kuwa upungufu wa huduma hizo.

Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya Chumba cha Mwalimu Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu Muktasi pamoja na ofisi za Msaidizi wa Mwalimu mkuu na walimu wote huku zikiwa na Vyoo vya kisasa pamoja na Bafu.

"Siwezi kuwa na amani kama walimu wangu hawana ofisi wala vyoo katika shule 402, ni aibu na fedheha kwa walimu kugombania choo na mwanafunzi au kutumia vyoo vya majirani au Bar, hii sio heshima ya mwalimu wa Mkoa wangu,ndio maana nimeamua kuanza kufanyia kazi changamoto hizi," Alisema Makonda.

Kutokana na gharama za ujenzi kuwa kubwa Mheshimiwa Makonda ameviomba vyombo vya Ulinzi na usalama vya Mkoa wa Dar es Salaam kumpatia mafundi wa ujenzi kama sehemu ya kuunga mkono jitiada alizoanzisha za ujenzi wa Ofisi hizo ambapo vyombo hivyo vimeridhia kumuunga mkono.

“Kipekee napenda kuvipongeza vyombo vyote ya Ulinzi vilivyoamua kuniunga mkono vikiongozwa na Mkuu wa JKT kwa utayari wa kunipa vijana watakaofanya ujenzi huo, na niwaeleze kuwa ujenzi utaanza baada ya wiki mbili zijazo” Aliongeza Makonda.

Ujenzi wa Ofisi hizo unategemea zaidi jitiada za wadau wa maendeleo ikiwemo wamiliki wa kampuni pamoja na Wananchi wenye dhamira ya kuona Walimu wanafanya kazi katika mazingira Mazuri.

Tayari jitiada za Mheshimiwa Makonda zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kupata Mabati 11,000 na mifuko ya Saruji 1,000 ambapo Mahitaji ni Mabati 50,000/= Mbao zaidi ya Million mbili pamoja na vifaa vingine vya ujenzi.

Makonda amesema ataanza kutembelea viwanda vinavyojihusisha na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemo Mabati, Saruji, Nondo na vinginevyo kuona namna wanavyoweza kuunga mkono ujenzi huo ili kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira rafiki.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAS MADENGE ASISITIZA UTOAJI HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI

    January 24, 2023
  • RC Makalla Kuwapeleka Safari ya Mafunzo Viongozi wa Bodaboda na Machinga Nchini Rwanda

    January 20, 2023
  • RC Makalla Atembelea Ujenzi wa Kituo cha Biashara Afrika Mashariki

    January 19, 2023
  • RC Makalla Achoshwa na Danadana za Mkandarasi Soko la Tandale

    January 19, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa