• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

MAELFU WAMWAGIKA KUTUMIA FURSA YA RC MAKONDA YA MSAADA WA KISHERIA

Posted on: January 29th, 2018

Zaidi ya Wananchi Elfu Tatu leo wamejitokeza ikiwa ni Siku ya kwanza ya Utatuzi wa Malalamiko ya Kisheria kwa Wananchi waliodhulumiwa chini ya Wanasheria Magwiji 160 ikiwa ni Mkakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kusaidia wanyonge waliodhulumiwa Mali zao kupata haki pasipo kuvunja sheria.

Wananchi hao wametaabika kwa muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao Walizochuma kwa tabu na sasa kupitia huduma ya Msaada wa Kisheria uliotangazwa na RC Makonda wanaamini watarejeshewa haki yao.

RC Makonda amesema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza leo inatoa picha kamili Kuwa wapo viongozi wasiotekeleza vyema majukumu yao ya kiofisi kwenye idara zao ambapo ameahidi kuwawajibisha.

Aidha RC Makonda amesema kilichomgusa kuandaa Wiki ya msaada wa kisheria ni baada ya kubaini uwepo wa wananchi wanaonyanyasiki na hata kufikia hatua ya kufa kwa presha au kupooza miili baada ya kudhulumiwa na watu wenye pesa au wanaotumia uelewa wa sheria kukandamiza wanyonge.

Kutokana na idadi kuwa kubwa ya wananchi wanaoendelea kujitokeza RC Makonda ameongeza wanasheria wengi zaidi ili kuhakikisha Kila anayefika na kupata namba anahudumiwa ipasavyo ambapo amewaomba wanasheria kuhakikisha wanawasikiliza wananchi kwa umakini na kuchambua nyaraka kwa ufasaha na wasitoe hukumu.

RC Makonda amesema katika zoezi hili limehusisha Wanasheria wabobezi, Wataalamu wa kutambua nyaraka zilizogushiwa, watendaji wa Ardhi na watumishi wa Mahakama ambao wapo kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi.

RC Makonda amesema baada ya kupokea ripoti kamili ya kesi zote atasimama kuhakikisha Hakuna mnyonge anabaki akinyanyasika.

Zoezi la kusikiliza wananchi waliodhulumiwa Mali zao ikiwemo Nyumba, Viwanja, Magari, Mirathi na Kazi litaendelea hadi siku ya Ijumaa ya Februari 02.

Nao wananchi waliojitokeza wamemshukuru RC Makonda kwa kutambua Tabu wanazozipata baada ya kudhulumiwa na wajanja ambapo wengine wamesema wamepoteza Waume, Wake zao na wengine kupata magonjwa baada ya kudhulumiwa na wametaabika Muda mrefu kutafuta haki pasipo kufanikiwa lakini kupitia utendaji kazi makini wa RC Makonda wanaamni haki inapatikana.

 

MWENYE HAKI AKITAWALA TAIFA HUSTAWI, TUMEMPATA RAIS MPENDA HAKI.

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Operesheni Panya Road Imekuwa na Mafanikio

    May 27, 2022
  • RC Makalla Asimamisha Shughuli za Uchimbaji Madini Boko - DSM

    May 26, 2022
  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa