• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Kilele cha Wiki ya Maji Duniani Mkoa wa Dar es Salaam chaadhimishwa Wilaya ya Ubungo

Posted on: March 22nd, 2018

Maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji Duniani  katika mkoa wa Dar es Salaam yameadhimishwa leo tarehe 22/03/2018 katika viwanja vya Mburahati barafu yakipambwa na matukio muhimu mawili ya Uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi mkubwa wa uchakataji maji taka na upandaji miti kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya ubungo amesema maadhimisho ya wiki hii ya maji kimkoa kilele chake kinaadhimishwa hapa kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uchakataji maji.

Lakini pia kwa kipindi cha wiki nzima tumekuwa tukishiriki katika shughuli mbalimbali tukikumbushwa namna bora ya kutunza vyanzo vya maji ili mkoa wetu wa Dar es salaam huduma hiyo ya maji ipatikane vizuri  na tuwe na maji ya kutosha na salama.

"Kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema hifadhi vyanzo vya maji na mifumo ya ikolojia kwa maendeleo ya jamii" Alisema Kisare.

Mgeni rasmi katika hotuba yake amesema amefurahishwa kusikia katika wiki hii ya maji mkoa umeshiriki katika shughuli za upandaji miti katika chanzo chetu kikuu cha maji ambacho ni mto Ruvu.

Pia utoaji wa semina na elimu juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira ili kuweza kuvilinda vyanzo vyetu viweze kuwa na maji wakati wote yatakayotuwezesha kukidhi mahitaji katika mkoa wetu.

Ujenzi wa mradi huu wa uchakataji maji taka kwa wakazi wa Mburahati utawasaidia kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.

Pia maji yaliyochakatwa yataweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga na uzalishaji wa gesi kwa matumizi ya majumbani.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam vyanzo vya maji vinavyotegemewa ni mto Ruvu na visima kwa sasa maji yanayopatikana yanakidhi mahitaji ya jamii kwa takribani asilimia 75 hivyo jitihada inafanyika kuweza kufikia asilimia 95 hadi 100 ifikapo mwaka 2025

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es Salaam Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na mwenyeji Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa