• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

KIKAO CHA (TASAF III) KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM CHAMALIZIKA LEO TAREHE 30/06/2017

Posted on: June 30th, 2017

KIKAO CHA WADAU WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI AWAMU YA TATU (TASAF III) KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM CHAMALIZIKA LEO TAREHE 30/06/2017 KWA MIKAKATI MIKUBWA KUWEKWA YA NAMNA YA KUWAHUDUMIA WALENGWA WA MPANGO.

Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa tarehe 28-30 Juni, 2017 na kuhudhuriwa na Waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, Wahasibu wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini, Maafisa Ufuatiliaji (TMO),Wafuatiliaji wa Utimizaji wa masharti ya Afya na Elimu (Maafisa Afya na Elimu Msingi na Sekondari) na Wataalamu wa Ngazi ya Mkoa.

Katika siku ya kwanza wadau hao wa mpango wa kunusuru kaya masikini walipata mafunzo ya mfumo wa malipo kwa njia ya Ki-ilekroniki “Electronic Payment System” ambapo walipata kuelewa kuwa mbali na malipo ambayo hufanyika kwa njia ya kawaida ya kupewa pesa mikononi lakini kuna njia nyingine za kutumia simu au akaunti zao za benki kuingiziwa pesa. Njia hii itasaidia walengwa wa mpango kupata malipo yao moja kwa moja wakiwa katika maeneo yao ya Makazi bila kwenda kwenye maeneo ya malipo.

Katika Siku ya pili, Wadau walijifunza umuhimu wa kuhuisha  taarifa za walengwa kwa kila Halmashauri kwenye mfumo wa Tasaf ambapo hapa walielezwa kuwa kila mlengwa asipohuishiwa taarifa zake hawezi kupata huduma stahiki hivyo kukosa kipato,fedha ya chakula,elimu na huduma za afya pia. Vilevile Wadau walihimizwa kuwa takwimu ndiyo nyenzo muhimu zitakazowasidia Watendaji na Wadau wengine kupima uelekeo wa Mpango huu.

Siku ya tatu wadau walipata fursa ya kujikumbusha maana halisi ya Mpango wa Kunusuru kaya maskini, lengo lake,walengwa wa mpango huo ni watu gani, changamoto katika utekelezaji wa mpango huo na kuweka maazimio ya namna ya kutatua changamoto hizo.

Katika kufunga Mkutano huo Mwenyekiti aliyeteuliwa na wadau hao katika kikao kazi hicho Bw. Hermeni J. Msia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa dhati wadau hao kwa kuhudhuria katika kikao kazi hicho kwa muda wa siku tatu bila kukosa na kuweza kujua mbinu mbalimbali za kwenda nazo katika kuwaahudumia walengwa vilevile aliwasisitizia wadau kwenda kufanya kazi kwa bidii bila kujali  changamoto zilizopo kwani mpango huo wa kusaidia kaya masikini umefanya mambo makubwa na ya muhimu kwa Taifa kama vile:-

  • Kuongezeka kwa kiwango cha mahudhurio ya watoto kwenye vituo vya Afya.
  • Kuongezeka kwa kiwango cha mahudhurio ya watoto shuleni
  • Kuimarika kwa hali ya maisha ya wanufaika (beneficiaries) wa mpango



Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa