• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam Yaridhishwa na Utekelezaji wa Miradi Kinondoni

Posted on: November 9th, 2023

 

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Dar es salaam chini ya mwenyekiti wake Komredi Abbas Mtemvu leo Novemba 9, 2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa Kinondoni katika majimbo ya Kinondoni na Kawe.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa akitokea Dar es salaam Juma S. Gaddafi alisema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anahangaika usiku na mchana kuwasaidia watu wanyonge na masikini hivyo ni wajibu wa kamati kupita na kukagua pesa zinazotolewa zinafanyiwa kazi inavyotakiwa na kamati iliridhia maendeleo yake.

Mhe. Gaddafi alisema, "Sisi tumefanya ziara kwenye majimbo hayo na miradi yake, tumeona pesa zinavyokwenda zinaenda vizuri na zinatumika kama zilivyoombwa, niwapongeze Mstahiki Meya na timu yake, wabunge wa Kinondoni na Kawe na wataalamu wote."

Naye mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ambaye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo alisema wamejikita kwenye afya, elimu  na barabara, "Sisi jukumu letu ni kusimamia miradi hiyo kwenye viwango, ili kuwe na thamani ya pesa  na pia kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, mfano miradi ya shule ikamilike kwa wakati na ibebe waanafunanzi kwa wakati na zaidi katika kiwango cha maghorofa kutoka na uhaba wa Ardhi Katika Mkoa huu, alisema.

Aidha RC Chalamila alieleza ujengaji wa madarasa na vituo vya afya kwa maghorofa  inasaidia kuzuia kusambaa kwa majengo kutoka ardhi ndogo ya mkoa wa DSM kutoka na wingi wa watu wake hivyo aliwapongea sana watendaji wote kwa malengo yaliyokamilishwa hali itakayorahisisha kueleweka zaidi kwa wapiga kura kipindi kijacho cha  uchaguzi 2025.

Miradi iliyokaguliwa kwa jimbo la Kinondoni ni miradi mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 4.325 ambayo ni ujenzi kituo cha afya, madarasa na vyoo shule ya msingi Mapinduzi, uwanja wa mpira na barabara (Mwenge), huku jimbo la Kawe miradi mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 2.799 nayo ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari Changanyikeni, nyumba ya mwalimu shule ya sekondari Godwin Gondwe na ujenzi wa mabweni, madarasa na vyoo Mbweni.

Miradi mingi imekamilika asiliamia 90 na ipo michache ambayo ipo kwenye hatua za mwisho, imechelewa kutokana changamoto mbalimbali ambayo ni asiliamia 10

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa