• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Halmashauri ya Ubungo Yaibuka Kinara Utoaji wa Huduma Bora za Afya DSM

Posted on: July 21st, 2022

Katibu Tawala Mkoa Ndg Hassan Rugwa akimkadhi Tuzo Dkt Peter Nsanya Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo kufuatia Wilaya hiyo kuibuka kinara katika utoaji wa huduma bora za Afya kati ya Halmashauri tano DSM


Katibu Tawala Mkoa Ndg Hassan Rugwa akimkadhi Tuzo Dkt Kiwelu Mganga Mkuu Hospitali ya Amana  kwa ushindi wa Hospitali hiyo katika utoaji wa huduma bora za Afya kati ya RRH zote DSM


Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati wameibuka washindi na Kupatiwa tuzo ya heshima katika utoaji wa huduma Bora za Afya Kati ya Halmashauri tano za Mkoa huo katika kipindi Cha mwaka 2021/2022.

Ubungo imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 237 ikifuatiwa na Halmashauri ya Temeke ikiwa na alama 236 na Halmashauri ya Kigamboni imeshika nafasi ya tatu kwa kupata alama 235.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao Cha Mwaka Cha Siku mbili kilicholenga kupata tathimini ya utendaji kazi wa sekta ya Afya Mkoa wa Dar es salaam, Katibu Tawala wa Mkoa huo Hassan Abbas Rugwa amepongeza sekta ya Afya kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika utoaji wa huduma Bora za Afya.

Aidha Rugwa ametoa zawadi kwa Hospital ya rufaa ya Amana kwa kushika nafasi ya kwanza Kati ya hospital tatu za rufaa kwa kupata alama 118 ambapo Hospital ya rufaa Temeke imeshika nafasi ya pili kwa kupata alama 107 hospital ya rufaa Mwananyamala imeshika nafasi ya tatu na kwa kupata alama 102.

Pamoja na hayo Rugwa ametoa zawadi ya vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika kipengele Cha uandaaji wa mipango ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeshika nafasi ya kwanza kitaifa ya kwanza kimkoa, ikifuatiwa na Halmashauri ya Kinondoni nafasi ya pili kitaifa na ya pili kimkoa na Kigamboni nafasi ya tano kitaifa na tatu kimkoa.

Hata hivyo Rugwa ametoa zawadi ya cheti kwa Amana Kituo Cha kuwahudumia Wagonjwa wa virusi vya UKIMWI pamoja na kwamba walifungiwa mwaka Jana Kutokana na UVIKO19 lakini bado wamefanya vizuri kuliko wengine huku akitoa vyeti kwa Ithibati ya kimataifa ya maabara kwa Hospital ya sinza Palestina, Hospital ya Mbagala rangi tatu, Hospital ya rufaa Temeke, Mwananyamala RRH, Amana RRH pamoja na hospital ya mnazi mmoja ambao Wameahinda kwa Mwaka huu.

Wakati huohuo Rugwa ametoa zawadi kwa Manispaa zilizofanya vizuri kwenye kipengele Cha Usafi wa Mazingira ambapo Hospital ya rufaa Temeke imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya pili kitaifa ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni iliyoshika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya tatu kitaifa



Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla, NMB Wakabidhi Ticket kwa Viongozi wa Machinga na Bodaboda

    February 03, 2023
  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa