• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

CHINA KUONGEZA NGUVU ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DSM

Posted on: September 9th, 2017


Balozi wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini leo tarehe 09/09/2017 amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.

Mhe Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda_wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani ni wenye vipato vya Chini ambao idadi kubwa hawawezi kumudu Gharama za matibabu nje ya mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali mfano wa Bima ya Afya.

Kutokana na Mkusanyiko huo wa Maelfu ya wananchi Mhe Balozi wa China amesema Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeamua KUUNGA mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda na kuanzia sasa na kuendelea serikali ya ya Jamhuri ya watu wa China itaungana na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kusaidia zoezi upimaji Afya BURE!kwa kufanya yafuatayo :-

1. Serikali ya China italeta Madaktari Bingwa kutoka China ambao wataungana na Madaktari wa Timu maalum ya Mhe Makonda ambao wamekuwa wakitoa huduma za upimaji Afya Bure hivyo Madaktari wa Tanzania wataungana na Madaktari wa China katoka kuendesha huduma ya Utoaji wa Afya Bure Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Serikali ya China itatoa vifaa vya kisasa vya UPIMAJI ambazo vitasaidia kuongeza kasi ya upimaji kwa watu wengi zaidi.

3. Serikali ya China ITAGHARAMIA dawa kwa watu wasio na UWEZO wa kumudu Gharama za ununuaji dawa mara baada ya kupimwa na kuandikiwa dawa.

Mhe Balozi wa China amewashukur wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kumuunga mkono Mhe Makonda hatua ambayo imeishawishi serikali ya China kusaidia katika zoezi hilo zuri lenye Malengo ya kutoa huduma bora za Afya kwa Wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEMSHUKURU balozi wa China kwa Niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukubali kuunga mkono Jitihada za kuboresha Afya za wananchi wake, ambapo amesema wazo hilo la kutoa HUDUMA ZA upimaji bure wa Afya alilianza tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya KINONDONI, na kumuhakikisha balozi huyo kuwa hilo litakuwa zoezi ENDELEVU kwa Mkoa wa Dar es Salaam likiwa na Malengo makubwa matatu ambayo ni :-

1. Kuongeza UELEWA kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa Upimaji wa Afya hata kama hawaumwi.

2. Kuwawezesha wananchi WANYONGE kupata huduma za AWALI za upimaji wa Afya ili kuwasaidia mapema katika hatua za AWALI kugundua matatizo yao.

3. Kubaini magonjwa ambayo husababisha VIFO katika hatua za AWALI.

Mhe Makonda amesema kwa ujumla hatua anazozifanya Katia Sekta ya Afya zinalenga kuunga mkono jitihada na kipaumbele cha Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika masuala ya Afya, na ni kwa sababu hiyo ameamua kuendelea kupambana na changamoto zilizoko kwenye Sekta ya Afya pasipo kusubiria fedha za Bajeti ambazo hata hivyo hazitoshelezi mahitaji halisi ya Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • RAS Nguvila Atoa Maagizo 14 kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

    May 16, 2025
  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa