• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke amemtembelea Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda tarehe 23/05/207

Posted on: May 23rd, 2017

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke amemtembelea Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda tarehe 23/05/207 na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Jiji la Dar es Salaam na London nchini Uingereza.

Katika mazungumzo yao Mhe. Paul C. Makonda na Bi. Sarah Cooke wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya Majiji makubwa mawili ya Dar es Salaam – Tanzania na London nchini Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko ambapo Mhe. Mkuu wa Mkoa ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.

Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya UTAMBUZI wa mifumo ya teknolojia ya Kamera za kisasa zitakazofungwa barabarani kwa ajili ya kusaidia USALAMA wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika  Jiji la London nchini Uingereza hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji wa UWEZO kwa maofisa wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matumizi ya mifumo hii.

Katika kukabiliana na changamoto ya MIGOGORO YA ARDHI Mkoani Dar es Salaam, Mhe. Paul C. Makonda ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo Maafisa Ardhi na Mipango Miji wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi jambo litakalosaidia kuondoa KERO YA UPATIKANAJI WA HATI PAMOJA NA VIBALI VYA UJENZI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Vilevie, katika mazungumzo hayo Mhe. Mhe. Mkuu wa Mkoa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania wamejadili suala la uanzishwaji wa JIJI LA FIKRA (BRAIN STORMING CENTER) kwa ajili ya kuwakutanisha vijana wabunifu kama ilivyo kwa Tech City ya Uingereza.

Katika kuhitimisha mazungumzo yao Mhe. Mkuu wa Mkoa Paul C. Makonda na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke kwa pamoja wamekubaliana kuzikutanisha timu za wataalamu kutoka London na Dar es Salaam za kukabiliana na majanga haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake Bi. Sarah Cooke amefurahishwa na jinsi Mkuu wa Mkoa anavyopambana na Vita ya Madawa ya Kulevya ambayo imeathiri nguvu kazi kubwa sana katika Jiji la Dar es Salaam na kumuhakikishia kuwa Serikali ya Uingereza inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Matangazo

  • FOMU YA KUHUISHA MAJUKWAA YA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI DSM November 09, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Makalla Apongeza Mahakama Utatuzi wa Migogoro kwa Usuluhishi

    February 01, 2023
  • RC Makalla Atoa Vipaumbele kwa Wakuu Wapya wa Wilaya za DSM

    January 31, 2023
  • RC Makalla Apiga Marufuku Biashara kwenye Barabara ya Mwendokasi Mbagala

    January 28, 2023
  • RAS MADENGE ASISITIZA UTOAJI HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI

    January 24, 2023
  • Tazama zote

Video

RC Makalla akagua ujenzi wa Kipande cha SGR- kuingia Bandarini DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa