• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Ilala MC
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Kunenge Afanya Ziara ya Kushtukiza Usiku wa Manane,Atoa Maagizo Mazito kwa Wakandarasi "Wazembe'

Posted on: October 17th, 2020


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kushtukiza Usiku wa manane kwenye miradi mitatu mikubwa ikiwemo ya Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti, Soko la Kisutu na ujenzi wa Stendi ya kisasa Mbezi Louis kujionea Kama agizo alilotoa la kufanya kazi usiku na Mchana linatekelezwa.

Akiwa kwenye ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti na Soko la Kisutu RC Kunenge amekuta agizo la kufanya kazi usiku na Mchana halijatekelezwa jambo linalopelekea Miradi hiyo kushindwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa na kuleta kero kwa wananchi.

Kutokana ukiukwaji wa maagizo hayo RC Kunenge ametoa maagizo matatu mazito kwa Manispaa ya Ilala ikiwemo kuhakikisha Mkandarasi anapigwa faini kwa kushindwa kukamilisha ujenzi ndani ya muda kwa mujibu wa mkataba, Kumchukulia hatua za kinidhamu  Msimamizi wa Mradi pamoja na kumuwajibisha Mhandisi Manispaa hiyo kwa kushindwa kusimamia kazi yake.

Aidha RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kumpatia mapendekezo ya jinsi gani watakamilisha miradi hiyo kwa haraka ili iweze kuwa msaada kwa wananchi.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametembelea ujenzi wa Stand Mpya ya Mbezi Louis na kukuta kazi inafanyika usiku na Mchana ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi na kuagiza Mradi ukamilike kabla ya mwishoni mwa mwezi November.

RC Kunenge amesema siku ya kesho October 18 jumla ya Makontena 13 yenye Vifaa vya Ujenzi wa Stendi ya Mbezi yaliyokuwa yamekwama bandarini yataanza kutoka baada ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara na Mamlaka ya Mapato TRA.

Sanjari na hayo ametoa Wito kwa taasisi zote za Serikali zinazohusika kufanikisha miradi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.

Matangazo

  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Serikali - AWAMU YA PILI January 08, 2021
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Ratiba ya Mtihani wa Kumaliza Kidato cha Sita (ACSEE) - 2020 June 12, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Makabidhiano ya ofisi

    February 22, 2021
  • RC Kunenge: Stendi Mpya ya Mabasi ya Mbezi Louis Kuanza Rasmi Novemba 30, Majaribio Novemba 25

    November 09, 2020
  • RC Kunenge Afanya Ziara ya Kushtukiza Usiku wa Manane,Atoa Maagizo Mazito kwa Wakandarasi "Wazembe'

    October 17, 2020
  • Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Akutana na Walimu,Awahakikishia kuwa Serikali Itaendelea Kulipa Malimbikizo Yote Wanayodai

    September 22, 2020
  • Tazama zote

Video

Kampeni ya Tahadhari Dhidi ya Mafuriko kwa Wanafunzi jijini Dar es Salaam
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa