JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
USHIRIKA:
 
Ushirika [ Nyumbani ] au
 
 
 

Idadi ya Vyama vya Ushirika

 
 
 

Mkoa wa Dar es Salaam una Vyama Vikuu vitatu (3) vikiwemo Chama kikuu cha mazao DARECU. Chama cha Viwanda na Chama Kikuu cha Akiba na Mikopo SCCULT (1992) LTD. Pia kuna Vyama vine vya ubia yaani Joint Ventures Enterprises ambavyo vimeandikishwa Kisheria.

 
  • DARECU ni Chama Kikuu cha Ushirika cha mazao ambacho ni muungano wa Vyama vya Msingi 23 kazi yake ni kushirikiana na Vyama vya Msingi kununua mazao ya wakulima na kusambaza pembejeo.
 
  • SCULT (1992) LTD ni muungano wa Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania, kazi yake ni kutoa ushauri na kuvisaidia Vyama vya Msingi vya Akiba na Mikopo katika kupata mitaji na mafunzo ya uendeshaji Vyama kwa Wanachama na Viongozi.
 
  • Vyama vya ubia ni muungao wa Vyama vya Ushirika vya kibiashara katika maeneo ya masokoni kuwasaidia kutoa elimu ya biashara na mitaji.
  • SACCOS ni Vyama vya Akiba na Mikopo ambavyo vinatoa huduma ya mikopo kwa Wanachama katika kupata mitaji ya kuendeshea biashara mbalimbali na kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi.
 
 
 
 
 

Hadi kufikia Novemba, 2008 Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika 631 vilivyoandikishwa Kisheria vikiwemo Vyama vya Akiba na Mikopo 462. Vyama 23 vya mazao (korosho) na 151 vikiwa Vyama aina nyingine mfano ujenzi wa nyumba viwanda na uvuvi.

 
 
 
Ukaguzi wa Mahesabu wa Usimamizi wa Vyama
 

Mkoa kupitia Maafisa Ushirika wake umeweza kufanya ukaguzi na usimamizi wa Vyama na kutoa ripoti kwa Wanachama wake kwa Vyama 179 dhidi ya Vyama vilivyo hai 356 hadi Juni, 2008 sawa na asilimia 50.3% ya Vyama vinavyofanya kazi.

 

 

 
 

Changamoto:

 
  • Upungufu wa watumishi, Mkoa una jumla ya Maafisa Ushirika 13 katika Wilaya zake tatu (3) na ngazi ya Mkoa Maafisa Ushirika wawili (2) ukilinganisha na Vyama 631 vilivyopo ambavyo vinahitaji usimamizi wa karibu ili niweze kutoa huduma bora zaidi kwa Wanachama.
  • Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kazi ya ugani kwa Maafisa Ushirika ni tatizo.
  • Na pia upatikanaji wa mikopo kutoka Taasisi za fedha kwa Vyama vya Ushirika ni kikwazo kwa maendeleo ya Ushirika.
 
 
     
     
 
         
 
Ushirika [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213