JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MAZINGIRA
 
[ Maliasili ] Mazingira [ Nyumbani ] au
 
 
 
Siku ya Mazingira Duniani

 

Kila mwaka Mkoa unashiriki katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambapo utekelezaji wa maadhimisho hayo huanza tarehe 01 Juni, na kila Halmashauri kushiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali za usafi na uhifadhi mazingira katika maeneo mbalimbali. Mwaka 2007/2008 maadhimisho ya kilele cha sherehe hiyo yalifanyika Uwanja wa mnazi mmoja katika Manispaa ya Ilala na mgeni Rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Waziri mkuu.
 

MRADI WA USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA BAHARI NA PWANI (MACEMP)
(Marine and Coastal Environment Management Project) 

 

Mradi huu ulibuniwa na Serikali ya Tanzania na kufadhiliwa na Benki ya Dunia

 
 

Maeneo husika – Visiwa vya Pemba na Unguja kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara katika Wilaya 10 za mwambao wa Pwani Dar es Salaam ikiwa mojawapo.Aidha mradi ulianza mwaka 2007 katika Halmashauri zote tatu za mkoa, na sasa unaendelea katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

 

Lengo kuu la mradi ni matumizi endelevu ya rasimali ya Ukanda wa Pwani na Bahari ili kuondoa umasikini kwa wakazi wa maeneo haya.

 

Maeneo ya utekelezaji ya Mradi wa MACEP ni yafuatayo:-

 
  • Usimamizi madhubuti wa Ukanda wa uchumi wa Bahari Kuu.
  • Usimamizi madhubuti wa mazingira ya Bahari na ya Ukanda wa pwani.
  • Uanzishaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii za Pwani. Utekelezaji wake utakuwa chini ya TASAF.
  • Uwezeshaji wa utekelezaji wa mradi kwa kuajiri watumishi na ufuatiliaji.

 

 
 
 
 
 
 
 
Eneo la Pwani ya Dar es Salaam
 

 

Matarajio ya mradi wa MACEMP ifikapo 2011 ni kuongezeka kwa mapato yanayokusanywa na Taasisi mbalimbali pamoja na kuongeza kipato cha wananchi wanaoishi Pwani ya Tanzania.
 
 
Usimamizi wa mradi upo kama ifuatavyo
 
  • Kamati ya Uendeshaji: Wajumbe wake ni Makatibu Wakuu wa Wizara zinazohusiana na malengo ya mradi.
  • Kamati ya Wataalamu imeundwa na Wakurugenzi wa Idara na Taasisi zinazohusiana na malengo ya mradi pamoja na wawakilishi kutoka Sekta Binafsi.
  • Timu za uratibu wa mradi zinaundwa na Watumishi kutoka Sekta mbalimbali zinazotekeleza mradi.
  • Kamati ya kuhakiki na kupitisha mapendekezo ya mradi ya wanajamii.
  • Timu za utekelezaji wa mradi katika Wilaya.
Watekelezaji wenza wa mradi.
Mradi unatekelezwa na wadau mbalimbali, ikiwemo Serikali Kuu, Halmashauri, Wilaya/Miji/Jiji, Mashirika ya Umma na yasiyo ya Kiserikali
     
     
 
         
 
[ Maliasili ] Mazingira [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158