| Utangulizi |
| |
Shughuli za hifadhi ya maliasili na mazingira katika Mkoa wa Dar es Salaam hufanyika katika Halmashauri zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni. Shughuli hizi hufanyika kwa kuzingatia sera ya Taifa mazingira ya mwaka 1997, Sheria ya mazingira ya mwaka 2004 (EMA-2004), Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2005, MKUKUTA, MKURUBITA, malengo ya millennia ya Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025. |
| |
| |
Aidha Mkoa pia unazingatia na kutekeleza mpango wa Taifa wa upandaji miti, siku ya Mazingira Duniani, miongozo na mikakati mbalimbali ya uendelezaji na uhifadhi wa maliasili na mazingira. Maliasili iliyopo katika Mkoa inahusisha misitu, bahari na madini. |
| |
| |
Misitu |
| |
| |
| Eneo la hifadhi ya misitu ni Ha. 3,610 kwa takwimu za mwaka 2007 ambapo mwaka 2005 ilikuwa ha. 588 na mwaka 2000 ha. 90 tu. Ongezeko hili linaonyesha kuwa jitihada za kuongeza hifadhi ya misitu katika Mkoa ni kubwa na za kuridhisha. |
| |
|
| Kuhusu upandaji miti, Mkoa unaendelea kuwaelimisha na kuwahimiza wadau mbalimbali kupanda na kuitunza miti katika maeneo yao. Wananchi katika ngazi ya Kaya wanahimizwa kupanda miti isiyopungua 5 ya matunda na kivuli. Nia ya Mkoa ni kupanda miti ya kutosha ili kuboresha mazingira ya Jiji kwa kuongeza Ukanda wa Kijani na kupendezesha Jiji (“City greening and beutification”). Aidha katika utaratibu huu aina ya miti mbalimbali hupandwa kila mwaka ikiwamo ya matunda, nishati na biashara. Maeneo yanayopandwa miti ni :- maeneo ya wazi, Barabara, makazi, maofisini/viwandani, kandokando ya mito, mabondeni, fukwe ya bahari na maeneo ya vyanzo vya maji. |
| |
Mkoa wa Dar es Salaam umejipangia tarehe 10/4 ya kila mwaka kuwa ni siku ya maadhimisho ya kilele cha Upandaji Miti Kimkoa badala ya tarehe Mosi Januari ya kila mwaka ambayo ni siku ya Upandaji Miti Kitaifa, hii inatokana na majira haba ya mvua katika Mkoa wetu kwa kipindi cha vuli. Aidha kila mwaka Mkoa unashiriki katika kuadhimisha kilele cha siku ya mazingira Duniani ambapo utekelezaji wa maadhimisho hayo huanza tarehe 01 Juni, na kila Halmashauri kushiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali za usafi na uhifadhi mazingira katika maeneo mbalimbali
|
| |
| Matarajio |
| |
Mkoa unatarajia kuendeleza msukumo wa hifadhi ya Maliasili ulio endelevu, uvunaji unaozingatia taratibu zilizopo na kupanda miti katika maeneo yote yaliyo wazi |
| |
| Utekelezaji wa upandaji miti msimu 2006/2007: |
| |
Katika kipindi cha mwaka 2006/2007 miti ipatayo 2,039,410 ilipandwa ambapo Manispaa ya Ilala ilipanda miti 134,210, Temeke 355,200 na Kinondoni 550,000 katika maeneo mbalimbali Mkoani ikiwa ni katika barabara, maeneo ya wazi, maeneo yaliyobomolewa ya wafanyabiashara ndogo, vyanzo vya maji, mabonde, viwanda na katika Kaya. Aidha agizo la kila Kaya kupanda miti mitatu au zaidi na kuitunza lilisisitizwa. |
| |
Utekelezaji wa upandaji miti msimu 2007/2008: |
| |
| |
Lengo la Mkoa lilikuwa ni kupanda miti 3,311,625 ambapo Manispaa ya Temeke miti 1,500,000, Ilala 112,625 na Kinondoni 1,5000,000 na utekelezaji halisi jumla ya miti 2,160,536 imepandwa Kimkoa |
| |
Soma zaidi Takwimu za hifadhi ya misitu iliyopo Dar es Salaam |
| |
| |
| Madini |
| |
Shughuli za madini katika mkoa wa Dar es Salaam zinahusisha uchimbaji mchanga, mawe/kokoto, vifusi na uzalishaji wa chumvi utokanao na maji ya bahari kwa njia ya mabirika na mionzi ya jua. Aidha, ufanisi na usimamizi wa madini unahitajika ili kuhakikisha kuwa uvunaji huo ni endelevu kwa vile madini mengine ukiondoa chumvi ni maliasili inayoweza kumalizika (finite resources).
|
|
Shughuli za uvunaji madini zinasimamiwa na sheria ya madini namba 5 ya mwaka 1998 na mining regulations za mwaka 1999. Hata hivyo wanaoendesha shughuli hizo baadhi wanazo leseni na wengine ni wachimbaji wadogo wadogo wasiokuwa na leseni. Baadhi ya wakazi wa hapa mkoani hujishughulisha na shughuli hii ya uvunaji wa madini ili kujipatia kipato na ajira. |
|
Hamashauri husika hutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli hiyo ya uvunaji ingawa hata maeneo mengine yasiyotengwa huvamiwa bila utaratibu na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira. Pindi yatokeapo matatizo kama hayo mamlaka husika za Manispaa huchukua hatua za kisheria ili kudhibiti hali hiyo. |
| |
| |
|
|
 |
Miti ya Mikoko kama inayoonekana katika eneo la fukwe - Mtoni |
| |
Hali ya uvuvi mkoa wa Dar es Salaam : |
| |
| |
Mkoa wa Dar es Salaam ni Mkoa mmoja wenye umuhimu wa pekee katika maendeleo ya uvuvi – Tanzania. Umuhimu wake unatokana hasa na nafasi yake katika biashara, uwezo wa kiuchumi, wingi wa watu na kuwepo kwa miundombinu bora ya usafiri.
|
| |
Maeneo: |
| |
| |
Katika uvuvi, Mkoa wa Dar es Salaam una maeneo mazuri ya uvuvi katika Bahari ya Hindi. Aina mbalimbali ya samaki huvuliwa. Pia kuna maeneo ya ufugaji wa samaki, kamba, kaa n.k. Aidha ulimaji wa mwani ni eneo mojawapo linaloweza kupewa umuhimu wake siku za usoni. |
| |
Viwanda
|
| |
| |
Kutokana na umuhimu wa Dar es Salaam kibiashara na mahali ilipo, viwanda vya kutengeneza mazao mbalimbali ya samaki na kuongeza thamani na kukidhi viwango vinavyohitajika katika masoko ya nje vimejengwa |
| |
Viwanda vinavyochakata/kuhifadhi na kusafirisha samaki ndani na nchi za nje ya Tanzania pamoja na shughuli nyinginezo zinazohusika na uvuvi; katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke:-
|
| |
| Na |
Jina la kiwanda |
Eneo kilipo |
Aina ya mazao |
| 1 |
Fruits
De-la-Mer |
Mbozi road |
Kamba Miti, Kamba Kocha, Sangara, vibua, Ngisi, pweza sato n.k. |
| 2 |
Asmara Trading |
Keko Mwanga |
Barafu, Kamba miti, Pweza, Ngisi, Vibua, Tasi, Changu, Sato |
| 3 |
Barafu chaguo la wavuvi |
Nyerere Road |
Barafu ya kuhifadhia samaki kwa wateja mbalimbali hapa Dar es Salaam. |
| 4 |
Fidha Hussein Co. Ltd. |
Vingunguti/
Nyerere
Road
|
Simbi na mabome |
| 5 |
Cool Storage Ltd. |
Gerezani |
Barafu kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya samaki |
| 6 |
Euro Cold Storage Ltd. |
Nyerere/
Mandela |
Barafu, Ubus, Dagaa, Pweza,Ngisi |
| 7 |
Shiloh Sea Foods Co. Tanzania Ltd. |
Mjimwema |
Kamba miti ,Kamba kochi, (Live lobsters) |
| 8 |
Fresh Sea Foods Co. Tanzania Ltd. |
Vijibweni |
Live Lobsters |
| 9 |
Malique International Tanyique Ltd. |
Mjimwema |
Kamba kocha-Hai,
Kamba miti-Hai, - Simbi
|
| 10 |
Kasanda Enterprises Ltd.
|
Kigamboni |
Live Lobsters, Crets Sqliels , Sangara |
|
|
| Ufugaji Nyuki: |
| |
| Mkoa unaendeleza jitihada ya hifadhi ya misitu ambayo inasaidia katika ufugaji wa nyuki wanaozalisha asali. Kutokana na hifadhi zilizofanyika, Mkoa kwa sasa unayo mizinga ya kisasa 714, ikiwa Kinondoni ni mizinga 516, Ilala 168 na Temeke mizinga 30. Mapato yatokanayo na asali iliyozalishwa yanasaidia kupunguza umasikini na mtu mmoja mmoja. Jumla ya Lt. 1,040 zenye thani ya shs.5,200,000 Zilivunwa msimu 2006/2007.
Aidha uhamasishaji wa jamii na elimu ya ufugaji wa nyuki iaendelea kutolewa. |
| |
|
| |
| |
|