UTANGULIZI |
| |
Maji ni rasilimali muhimu kwa maisha ya viumbe vyote na mendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote, ubora wa afya na wa mazingira vinategemea kuwepo kwa maji yakutosha na yenye ubora unaotakiwa.
Wingi wa maji yanayofaa kwa matumizi mbalimbali una kikomo. Kutokana na ukomo wa wingi wa maji yenye ubora na umuhimu wake kwa maisha ya kila siku, usimamizi na utunzaji wake lazima uzingatie uwiano wa matumizi yote kwa ujumla wake. |
| |
| HALI YA HUDUMA YA MAJI MKOANI |
| |
Mkoa wa Dar es Salam unapata maji kutoka mito na visima kwa matumizi ya nyumbani, viwanda, bustani, mifugo, usafi na Mazingira. Eneo kubwa linalopata maji linahudumiwa na Kampuni ya DAWASCO (Dar es salaam Water Supply and Sewerage Company) ambayo imepewa mkataba na Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam, DAWASA (Dar es Salaam Water Supply and Sewerage Authority). Maeneo yasiyo na mtandao wa DAWASA hupata maji kutoka visima vinavyoendeshwa na vyombo vya watumia maji, Taasisi na watu binafsi. |
|
Vyanzo vikuu vya maji ni mitambo ya Ruvu Juu, Ruvu Chini, Mtoni na visima virefu 1,100 na vifupi 238 vilivyopo katika Mkoa. Vyanzo vyote hivi huzalisha lita milioni 353 kwa siku zinazotosheleza asilimia 75% ya mahitaji ya lita millioni 469.3 kwa siku. Aidha, katika ngazi ya Jamii kuna Kamati za Maji 512 na Mifuko ya Maji 99. |
| |
| Malengo ya Kitaifa ni kuwapatia wakazi wa Mjini maji kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2010 na asilimia 100% ifikapo 2025. Kwa hiyo, bado tuko nyuma sana ukilinganisha na kiasi cha ukuaji wa Jiji na ongezeko la watu. |
| |
Huduma ya maji inayotolewa kwa wakazi wa Dar es salaam imekuwa ikiboreshwa kila mwaka.Mahitaji ya maji kwa Mkoa wa Dar es salaam yamefikia Lita 469,300,000 kwa siku yakijumuisha matumizi ya nyumbani ya Lita 352,300,000 na matumizi ya Viwanda, Kilimo, Mifugo, na usafi wa Jiji ya Lita 117,000,000 kwa siku. Kiasi cha maji yanayozalishwa ni Lita 353,000,00 kwa siku, ambapo DAWASA/DAWASCO inazalisha Lita 308,000,000 na Taasisi na watu binafsi lita 45,000,000. Hata hivyo mtandao wa DAWASA unapoteza Lita 128,000 sawa na asilimia 45 kila siku kutokana na ubovu wa mitambo, uchakavu wa mabomba na matumizi yasiyo halali. Hali hii inaendelea kudhibitiwa na DAWASA kwa kukarabati miundombinu yake, kuwawekea wateja mita za kupima kiasi cha maji wanayotumia, kuelimisha wananchi na kuchukua hatua za kisheria kwa wale wanaopatikana na makosa ya uharibifu wa miundombinu au wizi wa maji. |
|
| |
| |
| MAFANIKIO |
Hadi sasa Serikali imechimba visima virefu 653 na vifupi 219, imejenga miradi ya bomba 18 na kukarabati visima virefu 128 na vifupi 86. Aidha, Makampuni Taasisi na watu binafsi wamechimba visima virefu 457 na vifupi 19 na kufanya idadi ya visima virefu 1,100 na vifupi 238 jumla. Vivyo hivyo, wananchi na jamii Mkoa wa Dar es salaam wamehamasika na kuanzisha Kamati za maji 512 na mifuko ya maji 99. |
| |
|
| UTAFITI WA VYANZO VIPYA VYA MAJI: |
DAWASA inafanya utafiti wa kupata vyanzo vipya vya maji ya visima na mabwawa. Utafiti umefanyika eneo la Kimbiji ambapo kisima kirefu cha mita 213 kimechimbwa na kinatoa lita 300,000 kwa saa. Uchimbaji wa visima virefu umefanyika pia eneo la Mpera na Mpiji. Ili kutatua tatizo la upungufu wa maji kutoka Ruvu wakati wa kiangazi DAWASA inafanya utafiti huko Kidunda Morogoro ili wajenge bwawa la akiba kwa ajili ya kulisha mitambo ya Ruvu. |
| |
| |
| |
|
|
 |
Kisima Chenye pampu, Tanki na kituo cha kuchotea maji
|
| |
MIKAKATI YA KUENDELEZA HUDUMA YA MAJI |
| |
Njia zinazotumiwa kuboresha huduma ya maji ni kupunguza upotevu wa maji kwa kukarabati mitambo na mabomba yaliyopo kwenye mtandao wa DAWASA, kuongeza matanki ya kuhifadhia maji na kufunga mabomba mapya kwenda maeneo yasiyokuwa na huduma na kuchimba visima virefu. |
| |
Aidha mikakati ifuatayo pia inatekelezwa:- |
-
Kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali juu ya hifadhi ya mazingira na uendeshaji wa miradi ya Maji hususan ngazi ya Jamii.
-
Serikali kutafuta vyanzo vya fedha za kuendeleza miundombinu ya maji ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za kutosha toka vyanzo vyake.
-
Kufanya utafiti wa kupata vyanzo vipya vya maji juu na chini ya ardhi. Hadi sasa DAWASA wanachimba visima virefu Kimbiji, Mpiji na Mpera na usanii wa mradi wa ujenzi wa Bwawa eneo la Kidunda unaendelea.
-
Kuboresha miundombinu ya kusafisha na kusambaza maji kwa kukarabati na kuongeza mtandao wa mabomba, pamoja na kuwafungia wateja mita za kupima maji.
-
Kuunda vyombo vya watumia maji ili waweze kusimamia na kuendesha miradi yao ya maji katika ngazi ya Jamii.
-
Katika kuhudumia jamii Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wadau mbali mbali Miradi mikubwa ya maji inatekelezwa:-
a) Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji katika Mkoa wa Pwani na maeneo ya pembezoni ya Dar es Salaam unaofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia JICA. Mkoa utafaidika na US $ 5,987 ambazo zitatumika kati ya mwaka 2006 na 2008 kwa kuchimba vizima 12 na kusambaza maji.
b) Programu ya Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira(RWSSP) inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kuanzia mwaka 2007 hadi 2015 (Awamu ya Kwanza).
c) Miradi mingine inayofadhiliwa na Water Aid TASAF na Halmashauri za Manispaa.
|
| |
| |
CHANGAMOTO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI
|
| |
| |
Baadhi ya changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma ya maji ni pamoja na uzalishaji mdogo wa maji, uhaba wa vyanzo vya maji kutolipia huduma ipasavyo, ubadhilifu, uwezo mdogo wa watumia maji na gharama kubwa ya miundombinu ya maji. Aidha, Serikali inakabiliana na changamoto hizi kwa kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali na kutafuta vyanzo vya fedha za kuendeleza miundombinu ya maji |
| |
| |
|
| |
| |
| |
|