Eneo linalofaa kwa kilimo na ufugaji ni hekta 107,500, ambapo Manispaa ya Temeke ni hekta 55,000, Kinondoni hekta 37,000 na Ilala hekta 15,000. Hadi sasa eneo linalotumika kwa kilimo ni Ha.32,972 sawa na asilimia 31 ya eneo lote.
Hali hii inatokana na maeneo ya mashamba kutwaliwa kwa ajili ya kupimwa viwanja vya makazi na wawekezaji.
|
Mazao makuu yanayolimwa ni mihogo, viazi vitamu, mpunga, mahindi, migomba na kunde. Mazao ya biashara ni korosho, minazi, mboga, matunda, maua na viungo. Mkoa utoa kipaumbele katika kilimo cha mboga matunda na viungo (high value crops) ambayo yana soko la uhakika hapa Jijini. |
Msimu wa 2008/2009 lengo lilikuwa kununua tani 3,500 za korosho. Soko la korosho lilifunguliwa mwezi Oktoba na bei ya T.shs. 675 daraja la kwanza std. Na T.shs. 540 daraja la pili na ilitangazwa. Hali ya ununuzi ni mbaya, kwani Makampuni yaliyochukua leseni kununua korosho yamegoma kwa madai ya bei kubwa. |