- Kutoa huduma bora kwa wasafiri na watumiaji wengine.
- Kuondoa msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam uliosababishwa na mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kuegeshwa katika barabara za Msimbazi, Bibi Titi Mohamed (Mnazi Mmoja) na Morogoro (Eneo la Kisutu).
- Kuongeza mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
|
Kituo hiki kina ukumbwa wa Hekta 8.2. Kina uwezo wa kuhudumia wastani wa mabasi makubwa 350, madogo 70, wasafiri, wasindikizaji pamoja na watoa huduma mbalimbali kituoni wasiopungua 30,000 kwa siku. Sambamba na huduma za usafiri zipo pia huduma za kiuchumi zinazoendeshwa na Sekta binafsi, mfano Hoteli, maduka, karakana, kituo cha mafuta n.k. |
Kutokana na mahitaji ya huduma ya wasafiri kuongezeka, Halmashauri ya Jiji imepanga kupanua huduma za kituo hicho ili kiwe cha kisasa na kuendelea kutoa huduma bora zaidi. Umeandaliwa mpango wa biashara, (Business Plan) ambapo LAPF wataingia ubia na Halmashauri ya Jiji ili kuupanua mradi huo kwa kuanzia mwaka huu wa fedha 2008/09. Baadhi ya upanuzi utakaofanywa ni kujenga majengo marefu ya biashara zikijumuisha biashara ndogo ndogo, za kati na za daraja la juu, kuongeza huduma za mahoteli, vyumba vya malazi, ofisi mbalimbali na vituo vingine muhimu kama vya kubadili fedha n.k. |