Katikati ni Mganga Mkuu Hospitali ya Mwananyamala akiwa na Wataaalam kutoka Mkoani, walipotembelea Kituo kinachotoa huduma za UKIMWI Hospitalini hapo. |
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala huduma hii inatolewa katika kata 19 kati ya kata 22 zilizoko Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Mashirika yafuatayo:
Pathfinder,
CCBRT,
UMATI,
MDH.
|
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni huduma inatolewa kwenye kata zote 24 kwa kushirikiana na:
UMATI,
Action Aid Center ,
Pathfinder,
Matumaini Counseling Center ,
Kimara Peer Educators,
PASADA
|
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke huduma zinatolewa kwenye kata zote 27 kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yafuatayo;
UMATI,
PASADA,
TOH,
Pathfinder, na
Vuka Tanzania .
|
Mafanikio.
Mkoa wa Dar Es Salaam una zaidi ya NGO Mia sita zinazotoa huduma za UKIMWI na mkoa unashirikiana nao kwa karibu katika kuhakikisha ugonjwa huu unapungua au kutoweka.
Kuongezeka kwa vituo vya kupima na utoaji ushauri nasaha katika Manispaa zetu,
Kupungua kwa kasi ya maambukizi kutoka 10.9%(Tanzania Health Indicator Survey 2004) na kufikia asilimia 9.3 (KAMPENI 2007).
Kuundwa kwa kamati ya TB/HIV ya Mkoa.
Upo mpango wa utekelezaji wa TB/HIV ambao unaendelea kuutekeleza kwa ufadhili wa GF kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mafunzo yametolewa kwa watumishi wa afya wanaoshughulikia huduma za UKIMWI (counsellers).
Upatikanaji wa fedha za GF kwenye Manispaa zetu, Temeke ,Ilala na Kinondoni.
Lipo gari la Global Fund linalotuwezesha kufanya usimamizi kwa urahisi.
Wapo wafadhili wanaowezesha kazi hizi za UKIMWI zifanikiwe mfano MDH, G/F |