JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
Maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika
 
Siku ya Mtoto wa Afrika [ Nyumbani ]
 
 
 

Siku ya siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa tarehe 16, Juni ya kila mwaka. Siku hii inaadhimishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1976.

 

Lengo la Maadhimisho

Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto nchini Afrika ya Kusini wakati wakidai haki zao za msingi, pia kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla juu ya haki na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto. Aidha, hutoa nafasi ya kuwakumbusha watoto haki na wajibu wao kama watoto katika Taifa

 

Kauli Mbiu

Kauli mbiu ya mwaka huu (2011) inasema “Tuungane Pamoja Kuchukua Hatua za Haraka Kushughulikia Tatizo la Watoto Wanaoishi Mitaani”.

Bonyeza hapa kusoma zaid taarifa hii

 

 

 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
Siku ya Mtoto wa Afrika [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2860081/2863716, FAX: 022-2203213