JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
BIASHARA
 
Biashara [ Nyumbani ] au
 
  Baraza la Biashara la Mkoa na Wilaya
   
 

Baraza la Biashara la Mkoa limeanzishwa na kuzinduliwa Juni, 2007 chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na Wajumbe 40 wakiwemo 20 toka Sekta ya Umma na 20 kutoka Sekta binafsi kama ilivyoelekezwa na Waraka wa Rais Na. 1 wa Septemba, 2001

   
   
 

Kamati ya utendaji ya Baraza la Biashara la Mkoa inafanya kazi chini ya Uenyekiti wa Katibu Tawala Mkoa na mara ya mwisho imekutana 22/9/2008. Vikundikazi vine (4) vya Baraza la Biashara la Mkoa vimeundwa na vyo ni:-

  1. Miundombinu - Mwenyekiti Bw. Sabri Mabrouk
(Mwenyekiti DARCOBOA).
  2. Wajasiriamali na mitaji
  3. Ardhi - Mwenyekiti Eng. Kuzungu magilli Contractors Registration Board – TACECA).
  4. Uwezeshaji - Mwenyekiti Dkt. Donath R. Olomi (Mkurugenzi – EDC – UDSM).
   
   
 

Changamoto:

   
   
 
  • Bado Sekta binafsi haijaitikia vya kutosha kuhusu ushirikishwaji katika shughuli za uwekezaji, uendeshaji biashara na huduma za kiuchumi. Hata wakiitwa kwenye vikao vya Baraza la Biashara na shughuli zingine za kuendeleza ushiriki wao katika shughuli za uchumi hutaka kulipwa posho na Serikali.
 
 
  • Kitabu cha Fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam (Regional Profile) kimeshatayarishwa.
 
 
  • Mabaraza ya Biashara ya Wilaya yameanzishwa Juni, 2008 lakini
  Masoko:
   
 

Shughuli za masoko katika Mkoa wa Dar es Salaam zinayo nafasi kubwa hasa katika mauzo ya vyakula, vifaa vya ujenzi, umeme, nguo na vitu mchanganyiko.
Kuna jumla ya masoko 59 kama ifuatavyo:-
1. Temeke - 17
2. Ilala - 24
3. Kinondoni - 18

   
 

Masoko makubwa ni:-
Kariakoo, Buguruni, Ilala, Mchikichini, Temeke Stereo, Tazara, Kawe na Tegeta chini

   
   
 

Changamoto:

 
  • Wafanyabiashara wako wengi kupita uwezo wa masoko yaliyopo.
  • Serikali imeanza juhudi za ujenzi wa masoko kama Machinga Complex linalojengwa Ilala.
  • Inahitajika na Manispaa kujenga masoko hasa ya mtindo wa ghorofa pembezoni
   
 

Usafiri na Usafirishaji:

   
   
 

Mkoa wa Dar es Salaam unategemea sana huduma ya usafirishaji abiria kwa kutumia mabasi ya watu binafsi maarufu kwa jina la Daladala zisizopungua 6000.

   
   
 

Daladala hizo ziko za aina tatu.

 

(i) Magari madogo ya abiria 14 - 24
(ii) Magari ya abiria 25 - 34
(iii) Magari ya abiria 35 na kuendelea.

   
   
  Kila gari limeandikwa njia linalokwenda na rangi ya njia (route)imechorwa ubavuni ili kurahisisha utambuzi kwa abiria.
  Changamoto:
 
  • SUMATRA ndiyo inayotoa leseni, kudhibiti na kuratibu shughuli zote za Daladala. Lakini SUMATRA haiwajibiki kwa Mamlaka za Utawala zilizoko katika Mkoa wa Dar es Salaam.
  • Makondakta na madereva hukatiza routes mara kwa mara hivyo kusababisha usumbufu kwa abiria.
  • Makondakta na madereva hutakiwa kuvaa Sare na kuwa nadhifu na wasafi kila wakati lakini mara nyingi si wasafi.
  • Barabara nyingi ni finyu na hakuna njia za pembeni mwa Mji za kutosha (ring roads & pararell roads) hivyo kuna msongamano mkubwa wa magari asubuhi na jioni.
  Soko la Hisa
  Yafuatayo ni baadhi ya makampuni yaliyosajiliwa katika Soko la Hisa Jijini Dar es Salaam
  •  Tanzania Oxygen Limited
•  Tanzania Breweries Limited
•  Tanzania Tea Packers Limited
•  Tanzania Cigarette Company Limited
•  Tanga Cement Company Limited
•  Dar es Salaam Airport Handling Company Airways
•  Kenya Airways
•  East African Breweries Limited
 
Majengo pacha ya BoT
 
Viwanda:
 
 

Mkoa una viwanda vingi ambavyo huchangia katika kutoa ajira kwa Wananchi na kutoa mchango katika pato la Taifa.

Viwanda vya nguo ni pamoja na vifuatavyo:-

1. Karibu Tex tile - Mbagala

2. Nida Tex tile - Nyerere Road

3. EPZA Tex tiles - (Ubungo eneo la uwekezaji)

4. Urafiki Tex tile - Morogoro Road

 

Viwanda vya Bia na pombe kali ni:-

 

1. Tanzania Breweries - Ilala
2. Serengeti Breweries - Chang'ombe
3. Tanzania Distibaries - Chang'ombe
4. Chibuku

 
 

Viwanda vya soda ni:-

 
 

1. Cocacola kwanza Bottlers - Mikocheni

2. Tanzania Bottlers - Nyerere/Kiwalani

  • Viwanda vya Juisi ni pamoja na Azam Juice.
  • Viwanda vya mabati ni ALAF, MM STEEL na COTTEX Metals.
  • Viwanda vya mabomba na Nondo ni MM Steel, ALAF na SITA STEEL.
  • Kuna kiwanda kimoja tu cha saruji cha TPCC – Wazo Hill.
  • Pia kuna Makampuni makubwa yanayofanya biashara ya kuagizamagari na vipuri kama CMC, TOYOTA, AFRI CARRIERS Mkoa n.k
Biashara Nyinginezo

Mkoa una Hoteli za Kitalii, Bar, Migahawa na Maduka ya Jumla/nusu jumla, maduka ya reja reja na maduka ya madawa ya binadamu na mifugo.

 
 
Vitega Uchumi Vikubwa vya aina ya Pekee
 
 

Mkoa wetu una vitega uchumi vikubwa vya aina ya pekee kwa ukubwa na mapato Ki-Taifa ingawa mkoa haushirikishwi ipasavyo. Vitega uchumi hivyo ni:-

1. Uwanja wa Taifa

2. Uwanja wa ndege wa Mwalimu J. K. Nyerere

3. Bandari ya Dar es Salaam

4. Viwanja vya maonyesho vya Mwalimu J. K. Nyerere- Kilwa Road

 
 
Huduma za Kibenki
 

Huduma za kibenki katika Mkoa wa Dar es Salaam ni za kutosha na uhakika. Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) yapo Jijini Dar es Salaam, zipo Benki za Biashara, Maduka ya Kubadilisha Fedha za kigeni (Foreign Exchange Bureau), Makampuni ya Bima (Insurance Companies). Baadhi ya benki za biashara ni kama vile:NBC, NMB, CRDB, Postal Bank, Barclays, Standard Chartered (T) Limited, Kenya Commercial, Akiba, Stanbic, Exim, Citibank, FBME Bank, Euro African, Diamond Trust, International Commercial Bank, Habib African Bank, African Banking Corporation, United Bank of Africa, CF Union Bank Savings and Finance Commerce Bank, Azania Bancorp, TIB, Twiga Bancorp Limited, Baroda na Dar es Salaam Community Bank ambayo inamilikiwa kwa pamoja na Halmashauri ya Jiji na Halmashauri za Temeke, Kinondoni na Ilala.

         
 
Biashara [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158