Mkoa wa Dar es Salaam, unasimamia Sekta ya Ujenzi kwa kufuata sera zinazoongoza Sekta hiyo. Sera hizo ni sera ya ujenzi ya mwaka 2003 na sera ya uchukuzi ya 2000. Sera zote zinataka kuwa na ustawi wa sekta ambayo inajumuisha Barabara na Majengo.