| BARABARA |
| |
Mtandao wa barabara za Mkoa wa Dar es Salaam una urefu wa km 2094.4 ambapo kati ya hizo TANROADS inasimamia na kuhudumia barabara zenye urefu wa km 494.3 na zilizobaki km 1600.1 ziko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4). Halmashauri ya Jiji haina barabara inayoisimamia. |
| |
| |
| |
| Mtandao wa barabara umegawanyika katika makundi yafuatayo: |
Barabara kuu (Trunk roads):
Barabara kuu zote ambazo ni barabara za Morogoro, Kilwa, New Bagamoyo, Nyerere/Pugu,na Mandela/Sam Nujoma zina urefu wa km 126.2 |
|
Barabara za Mkoa (Regional Roads):
Barabara za Mkoa zote zinazosimamiwa na TANROADS zina urefu wa km 368.3
|
| |
| |
Barabara zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa |
Barabara za Halmashauri (District & Feeder roads)
Barabara za Halmashauri ni zile zenye urefu km 1600.1 zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4). |
| |
|
Jedwali la Mtandao na Aina za Barabara Mkoani
Dar esSalaam |
| |
Msimamizi |
Urefu wa Barabara(km) |
Aina ya barabara(km) |
| Lami |
Changarawe |
Udongo |
| Tanroads |
494.3 |
211.4 |
282.9 |
| Ilala |
429 |
132 |
80 |
217 |
| Kinondoni |
692.7 |
114.7 |
315.25 |
262.752 |
| Temeke |
478.4 |
67 |
411.11
|
| Jumla |
2094.4 |
525.1 |
1569.3
|
|
|
| |
Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara Mkoani |
| |
Kwa kushirikiana na Shirika la Msaada la JAPAN (JICA) mpango kabambe wa usafiri na usafirishaji umeandaliwa. Mpango huu utatumika katika uendelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu na aina mbalimbali za usafiri na uchukuzi hadi mwaka 2030. |
| |
| Barabara kuu inasimamiwa na TANROADS |
| |
Mkoa kwa kupitia wadau wake unaendelea na miradi wa ujenzi na ukarabati na barabara kuu kama ifuatavyo |
| |
| |
Ukarabati wa Barabara ya Kilwa (Km 12) awamu ya pili:
Kazi hii inafanywa na Kampuni ya KAJIMA ya Japan. Kazi inahusu upanuzi wa Barabara toka njia mbili za sasa hadi njia nne kutoka katika makutano ya Barabara ya Bandari hadi Mbagala Rangi Tatu.
Ukarabati wa barabara ya Mandela (km 16.5)
Kazi hii inafanywa na Kampuni ya Maltauro- Spencon- Stirlinga Joint Venture. Kazi inahusu ukarabati mkubwa wa Barabara kutoka Kurasini (Bandarini) hadi Ubungo
|
| |
| |
| Barabara zinazosimamiwa na Halmashauri ya Jiji na Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke |
| |
| |
| Halmashauri ya Jiji |
| |
| |
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam husimamia na kusanifu miradi ya ujenzi Wa barabara, taa za barabarani na mifereji ya maji ya mvua kwa kushirikiana na Manispaa zake inapobidi. Aidha inashughulikia barabara za ndani ya Kituo cha Mabasi Ubungo na kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa barabara zinazojengwa kwenye Makazi duni na yasiyopangwa (Unplanned Settlements) katika Manispaa za Ilala, Temeke, Kinondoni. |
Halmashauri ya Jiji inatekeleza miradi ya barabara chini ya mpango wa CIUP (Community Infrastructure Upgrading Programme) awamu ya kwanza (Phase I) kwa gharama za Tshs.6,496,362,371/= na kiasi cha Tshs.6,368,239,206.25/= Kwa awamu ya pili. Ujenzi huo unahusisha mifereji ya maji mvua, vizimba vya taka, uwekaji wa taa za barabarani (streets lights), njia za wapita kwa miguu na vyoo vya umma. |
|
| |
|
| |
|
|
 |
| |
| |
Halmashauri ya Manispaa Ilala |
Manispaa ya Ilala inahudumia barabara zenye urefu wa kilomita 427.99 ambazo kati ya hizo kilomita 132 ni za lami, kilomita 79.7 ni za changarawe na kilomita 216.92 ni za udongo. Katika mwaka wa fedha 2008/09 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetengewa jumla ya Tshs 1,030,000,000.00 kutoka Mfuko wa Barabara kwa ajili ya matengenezo (maintenance) ya barabara. Halmashauri pia imetenga jumla ya shilingi 3,022,000,000.00 kutoka vyanzo vyake kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ujenzi wa barabara.
|
|
| |
Halmashauri ya Manispaa Kinondoni |
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ina jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 681.252 ambazo kati ya hizo kilometa 120.42 ni za kiwango cha lami, kilometa 450.38 ni za kiwango cha changarawe na kilometa 110.452 ni za kiwango cha udongo.
|
| |
Katika mwaka wa fedha 2008/2009 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia vyanzo vyake vya ndani imetenga jumla ya Tsh. 933,779,000.00 kwa ajili ya uimarishaji wa miundombinu ya barabara na mifereji. Kati ya hizo Tsh. 563,779,000.00 ni kwa ajili ya ukarabati wa sehemu ya barabara ya Mikumi kwa kiwango cha lami na Tsh. 370,000,000.00 ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa mifereji ya maji ya mvua. |
| |
| |
Halmashauri ya Manispaa Temeke |
Manispaqa ya Temeke ina mtandao wa barabara zenye urefu wa km 943. kati ya hizo barabara zenye urefu wa kilometa 259 zinamilikiwa na kuhudumiwa na wakala wa barabara nchini Tanroads na barabara zenye urefu wa kilometa 684 zinamilkiwa na kuhudumiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Vile vile kati ya Kilometa 943, kilometa 169 ndizo zimejengwa kwa kiwango cha lami, kilometa 325 ni za changarawe na km 452 ni za udongo. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inahudumia barabara zake kwa kutumia fedha kutoka mfuko wa barabara na kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani.
|
| |
Kwa mwaka wa fedha 2008/2009 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi 114,000,000 Kutoka katika vyanzo vyake vya ndani ili kuhudumia barabara zake zenye urefu wa km 100 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kawaida na uimarishaji wa maeneo korofi katika kata zote za Manispaa. Pia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepanga kuanza ujenzi wa barabara Mbagala/ Mtonikijichi 1.5 kwa kiwango cha lami, Hatua iliyofikiwa ni kutangaza zabuni. |
|
Mradi wa barabara vijijini
|
| |
| Kwa mwaka wa fedha 2008/2009 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi 92,000,000/= Kupitia mradi wa usafirishaji vijijini kwa ajili ya ujenzi wa daraja la vumilia kooni linalounganisha kata za Kisarawe II na Somangira. Kazi hii imepangwa kufanyika robo ya tatu 2008/09 |
| |
Miradi ya Barabara kwa mwaka wa fedha 2008/09 ni kama ifuatavyo : |
| |
.Mkoa unategemea kutumika katika matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2008/09 zaidi ya shilingi bilioni 46. Fedha hizo zikiwa ni pamoja na bajeti ya Mkoa na fedha shilingi bilioni 20 ambazo ilizopewa na Serikali kwa ajili ya mradi maalum wa matengenezo ya barabara ili kupunguza kero ya msongamano wa magari Jijini. |
| |
. |
|
| |
| |
| |
|