JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
ARDHI
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Nyumbani ] au
 
 
Utangulizi
 

Utekelezaji wa Mipango ya Ardhi Mkoani Dar es Salaam

 

Jiji kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameandaa mpango wa muda mrefu wa uendelezaji wa Jiji.

 
Kuanzisha miji midogo pembezoni mwa Jiji
(Satellite towns)
.

 

Maeneo yanayotarajiwa kuanzishwa Miji hii midogo ni pamoja na :-
•  Eneo la Pugu Kajiungeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
•  Eneo la Kongowe, Mji Mwema na Kimbiji katika Halmashauri ya Temeke.
•Eneo la Luguruni na Bunju katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
Mpango huu umeanza kutekelezwa kama eneo la mfano huko Luguruni katika Manispaa ya Kinondoni. Eneo la Luguruni lipo kilometa 28 toka katikati ya Jiji na lina ukubwa wa hekta 75.5.

Aidha maeneo mbalimbali ya wazi na fukwe za bahari zinaendelea kuboreshwa ili kuleta mandhari nzuri ya jiji.

 
Uendelezaji upya maeneo Kongwe

Mipango mbalimbali imeandaliwa ili kuendeleza upya
(Re-development Plan) maeneo kongwe.
Uendelezaji upya wa maeneo yafuatayo umeshaanza na unaendelea kama ifuatavyo-.

•  Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Ni maeneo ya Kariakoo, Upanga na Ilala

•  Halmashauri yaManispaa ya Kinondoni
Magomeni kwa awamu ya kwanza ni Magomeni kota , na Kinondoni Kota na Masaki

•  Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Maeneo ni Kurasini , Temeke na Kigamboni

 

Uboreshaji makazi duni chini ya mradi wa Cities Alliance

 

Cities Alliance ni mpango wa kuboresha makazi duni katika Jiji la Dar es Salaam. Makazi duni ni yale yaliyopangwa na yasiyopangwa ambayo hayana huduma za msingi. Mpango huu unatekelezwa kulingana na mpango wa Millenium ambao unatekeleza lengo Na.7 kigezo Na.11.

 
 

Uendelezaji wa Miji Salama “Safer Cities Programme”

 
Halmashauri ya Jiji ipo katika Upangaji na utekelezaji wa Mpango wa Miji Salama ili iweshe kukalika, kuwekezeka na Amani
 
 
 

 

 
Moja ya maeneo ya makazi yasiyopangwa

 

Mradi wa uboreshaji wa Miundo mbinu kwenye maeneo yasiyopangwa kwa kushirikisha jamii "CIUP "

 

Mradi wa kuboresha miundombinu kwa kushirikisha jamii umianzishwa mwaka 2000. Mradi huu unatekelezwa na Halmashauri ya jiji pamoja na Halmashauri za manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke

Dhana ya Mradi :
Dhana ya mradi huu ni ushirikishwaji wa wananchi katika kuamua, kupanga, kutekeleza, kusimamia, kutathmini na kuendeleza shughuli za kuboresha mazingira katika maeneo yao.

 

 
Mradi huu ni moja ya miradi iliyo chini ya "Local Government Support Project(LGSP) na unatekelezwa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza imeanza kutekelezwa mwaka 2005 kwa kuhusisha Kata ya Buguruni (mitaa ya madenge, Mnyamani na Malapa) na Kata ya Vingunguti (mtaa wa Mtambani) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Kata yaManzase katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, (mitaa ya Muungano, Midizini, Uzuri, Kilimani, Mvuleni na Mnazimmoja); Kata ya sandali(mitaa ya Mpogo, mwembeladu na sandali) na Kata ya Chan'gombe A,B na Toroli) katika Halmashauri ya Manispaa ya Teemeke.
 
Awamu ya pili itahusisha Kata ya kigogo na Mtaa wa Mwananyamala kwa Kopa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Kata ya vingunguti katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Kata za keko na Azimio katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
 
Jumla ya wakazi 330,000 wa Jiji la Dar es Salaam watanufaika na mpango huu. Utekelezaji wa mpango huu umeanza mwaka 2005 na utaisha mwaka 2008 aidha utekelezaji wa awamu ya pili utaanza mwaka 2008-2011.

 

 
 
 
 
 
     
 
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Ramani ] [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158