JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
   
     
AFYA
 
Afya [ Rudi nyumbani ] au
 
 
Utangulizi
 

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa Dar es Salam ulikuwa na idadi ya watu wapatao 2,487,288 ambao wanaishi kwenye mitaa ipatayo 387. Idadi hii ya watu inapata huduma za afya kinga na tiba kupitia vituo vya kutolea huduma vya Serikali, Mashirika ya dini na yasiyo ya Kiserikali na Sekta binafsi. Kuna jumla ya Hospitali 27 ambapo za Serikali ni 4 na mashirika ya dini, NGO's na binafsi ni 23. Vile vile, kuna Vituo vya Afya vya Serikali 5 na binafsi, Mashirika ya dini na NGO's 18. Zahanati zilizopo ni 67 za Serikali na 305 za binafsi/mashirika ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali. Hata hivyo, kuna upungufu wa Hospitali 4, vituo vya afya 25 na zahanati 48 ili kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya watu waliopo Mkoani.

 
 
 

Sekta ya Afya katika ngazi ya Mkoa/Jiji inaongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa/ Jiji akisaidiwa na Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa (RHMT).

 

 

Aidha, Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya vituo 466 vya kutolea huduma za afya zikiwemo za Serikali, Dini, mashirika ya Umma na watu binafsi kama jedwali lifuatalo linavyoonyesha:-

 
 
NGAZI SERIKALI WATU BINAFSI JUMLA
Hospitali 5 23 28
Vituo vya Afya 5 24 29
Zahanati 84 305 389
Jumla 94 352 446

* Hospitali moja ni ya rufaa Muhimbili.

 

 

 
 
 
Uanzishwaji wa Hospitali Teule ya Mkoa:
 
 
 
Mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu hauna Hospitali ya Mkoa. Hali hii imesababisha msongamano mkubwa wa wagonjwa katika hospitali za Halmashauri za Manispaa na pia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
 

Jitihada za Mkoa katika kukabiliana na tatizo hili zinaonesha mafanikio ya kuridhisha baada ya uongozi wa Hospitali ya “Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania ” (CCBRT) ambayo imekuwa ikitoa huduma za tiba ya macho tu kukubali kushirikiana na Serikali kuibadilisha Hospitali hiyo kuwa Hospitali Teule ya Mkoa.

 
 
Jitihada hizo zimefikia hatua ya kusainiwa Mkataba wa makubaliano ya uendeshaji wa Hospitali Teule ya Mkoa. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 24 Novemba, 2007 kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Uongozi wa CCBRT.
 
 

Kwa mujibu wa Mkataba huo, CCBRT itahusika na upanuzi wa hospitali iliyopo kwa kujenga majengo mapya yanayokidhi mahitaji ya kiwango cha Hospitali Teule ya ngazi ya Mkoa na kukarabati majengo yaliyopo. Serikali itahusika na ajira ya watumishi na kulipa mishahara ya watumishi.

 
 
Mkataba huo ni wa miaka mitano (5) tangu siku ya kusainiwa na Mkataba huo unao uwezekano wa kurudiwa (renewable). Hatua iliyokwishatekelezwa na Serikali ni pamoja na kutenga fedha za mishahara TShs.692,604,000 katika mwaka 2007/08.
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
         
 
Afya [ Rudi nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158